MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa anaungana na watanzania wote kumpongeza Rais wa Jamhuri ya kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Aftika (SADC).

Magufuli amerithi mikoba ya kiti cha Uwenyekiti wa SADC kutoka Kwa mtangulizi wake Rais wa Namibia, Dr. Have Geingob na atadumu na cheo hicho Kwa mwaka mmoja. 

Makonda amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kumpa pongezi Magufuli kutokana na kuaminiwa Kwa utendaji wake wa kazi. 

"Kwetu Sisi tunaona fahari Kwa kiongozi wetu kupewa jukumu la kuongoza nchi 16 zilizo ndani ha SADC ni matokeo ya uzalendo nasi tunapaswa kuendeleza uzalendo Kwa vitendo.

"Tuna jukumu la kuendeleza uzalendo ambao uliachwa na Mwalimu Julius Kambarange Nyerere ambaye ni mmoja wa waasisi wa Jumuiya hii kwa kuwasaidia wengi kupata Uhuru, hatuna bundi kuungana na kiongozi wetu ambaye Kwa sasa ana jukumu la kuendeleza Yale yaliyoachwa na waasisi hasa malengo yake makubwa yamekuwa ni kutotoa kwenye Lindi la umaskini.

"Kama ambavyo amesema kuwa Mataifa yetu si maskini na namna jitihada zilivyotumika kuwatoa wengi kwenye utumwa hizo ndizo zitatumika kuyatoa Mataifa yetu kwenye dimbwi la umaskini kama alivyosema kwenye hotuba yake, ni wakati wetu wa kuungana na kumpa sapoti,".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...