Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kuweka mikakati ya kuimarisha hali ya lishe katika ngazi ya jamii ili kupunguza hali ya udumavu kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwenye kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini hapo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwe na taifa lisilo na kiwango cha chini cha hali ya lishe waganga wakuu hao lazima wapange mikakati ambayo itaanzia ngazi ya jamii ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa lishe bora na inayostahili kwa familia hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili mikakati hiyo ifanikiwe.

Hata hivyo alisisitiza watoa huduma kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuimarisha huduma za afya katika maeneo yao ili wananchi wanaoenda kupata huduma wapate huduma hizo kwa haki na usawa" na katika hili ni vyema mwananchi anayekuja kupata huduna ni vyema aridhike na huduma anayopata katika vituo vyetu vyote nchini”.Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliwataka waganga wakuu hao kusimamia utendaji wa kazi katika maeneo yao ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii“inasikitisha kuona mama mjamzito anafariki kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uzembe au kutokupata huduma sahii jambo hili halikubariki”.

Kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri mwaka huu kinafanyika jijini hapa ambapo kilifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na kauli mbiu ya kikao hicho ni “Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati na utakua wa siku tano.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...