Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAKILI wa kujitegemea na Mshauri Msaidizi wa masuala ya kisheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Albert Msando amekabidhi fedha Sh.milioni tano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Fedha hizo zilikuwa ni ahadi ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kwa ajili ya matibabu ya marehemu Sabina kitwae Loita aliyefariki dunia hospitalini hapo na mtoto wake kushindwa kulipa gharama hizo na hivyo akamuomba Rais msaidie kulipa na Rais alikubali kukulipa gharama hizo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo Wakili Msando amesema aliamua kutumia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuhamasisha ndugu jamaa na marafiki kuchangia fedha hizo.
"Kuna sababu kuu tatu zilizosababisha kuchangiasha fedha hizi ikiwemo kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ya kijamii pamoja kuona mahitaji mengi na ninawasihi wote tutakaoguswa na kuwasaidia wagonjwa tufike Hospitali ya Muhimbili na kuchangia kile ambacho tumejaliwa" ameeleza Wakili Msando.
Pia amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma kufanikisha kupatikana kwa fedha hizo ni kumsaidia Rais ambaye ana majukumu mengi na wanaomlilia ni wengi.
" Rais Magufuli alipokuja Muhimbili kuwaona wagonjwa waliopata ajali ya moto mkoani Morogoro na akakutana na mama aliyempoteza mama yake mzazi na kushindwa kulipa bili ya Sh.milioni tano.
"Aliuambia uongozi wa hospitali "Nidaini mimi" hivyo basi kwa kuwa Rais ni binadamu na ana majukumu mengi hivyo tukaona tulibebe hili" ameeleza Msando.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrance Museru amesema kuwa gharama za matibabu ni ghali sana na ni haki ya kila mwananchi kupata matibabu.
"Ni vema wananchi wajiunge na mifuko ya bima ya afya kwa kuwa watanzania wenye mahitaji ni wengi na tunawaomba wadau wajitokeze kwa wingi kwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 500 hadi 600 hufutwa kwa mwezi kutokana na hali za kiuchumi za wananchi,"amesema.
Profesa Museru amesema kuwa waliandika barua Ikulu baada ya Rais kuchukua deni hilo na baada ya deni hilo kulipwa leo wataandika barua tena kwenda Ikulu ambayo itaeleza deni lililobaki.
Aidha amemshukuru Msando kwa kuona mahitaji ya hospitali hiyo na kutumia vyema mtandao wa kijamii kuhamasisha wananchi kuchangia gharama hizo za matibabu.
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya taifa Muhimbili profesa. Lawrance Museru (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea fedha hizo za malipo kwa matibabu za Sabina Kitwae Loita ambaye alifariki dunia hospitalini hapo zikizochangwa na wananchi na kuwasilishwa na wakili wa kujitegemea na mshauri msaidizi wa masuala ya kisheria wa CCM Albert Msando (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.
Wakili wa kujitegemea na Mshauri msaidizi wa masuala ya kisheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Albert Msando (kushoto) akimkabidhi fedha taslimu za kiasi cha shilingi milioni tano ambazo ni gharama za matibabu ya Sabina Kitwae Loita ambaye alifariki dunia hospitalini hapo kwa Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Profesa. Lawrance Museru leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...