Na. Catherine Sungura, Dodoma 

Wauguzi wote nchini wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja na kuacha tabia za ubinafsi ili kuweza kuwasaidia wananchi wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata huduma bora na kwa wakati. 

Hayo yamesemwa na katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula aliposhiriki kikao cha kuwashirikisha wadau mwongozo wa utoaji huduma kwa kuzingatia utu,heshima na maadili kilichofanyika jijini hapa. 

Dkt. Chaula alisema kuwa taaluma ya uuguzi ni ya wito hivyo wanatakiwa kuzingatia weledi wa fani yao ili kuwa na mafanikio ya utoaji huduma za afya nchini ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wanahitaji msaada wa kuokoa kutoka kwa wataalam hao. 

“Lazima turudishane kwenye mstari ili tuweze kuokoa maisha ya akina mama wajawazito,watoto na wagonjwa wengine ,tujiulize kwanini akina mama wajawazito wanafariki?nyinyi ndio chachu ya mabadiliko katika utoaji wa huduma”.Alisisitiza Dkt.Chaula. 

Aidha, katibu mkuu huyo alisema kuwa katika kutimiza wajibu wa wauguzi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya anatamani kusiwepo na kifo hata kimoja hususani upande wa akina mama wajawazito hivyo inahitajika nguvu ya pamoja na uelewa miongozi mwa wauguzi kote nchini ili ifikapo 2020. 

Mkakati wa kitaifa wa kupunguza vifo wa vitokanavyo na uzazi tanzania imekusudia ifikapo mwaka 2020 kupunguza vifo hivyo kufikia 292 katika vizazi hai laki moja ukilinganisha na mwaka 2015 vya vifo 556 kwa vizazi hai laki moja.

washiriki wa kikao cha wadau cha kuwashirikisha muongozo wa utoaji huduma kwa kuzingatia utu,heshima na maadili ya wauguzi nchini

Bi. Jane Mazigo kutoka baraza la wauguzi tanzania akichangia kwenye kikao hicho.

Aliyekua mganga mfawidhi wa zahanati ya uturo Wilson Chotamganga akielezea jinsi kijiji cha uturo kilivyofanikiwa kuondoa vifo vitokanavyo na uzazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...