Moureen Tesha, Kasulu. 

Wakulima wa zao la tangawizi wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wameiyomba serikali kuongeza nguvu katika zao hilo kutokana na kuwa jipya katika mkoa huo. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya NOJEPACO CO LTD ya jijini Arusha, wakulima hao wamesema ipo haja ya ya serikali pamoja na mambo mengine kuhakikisha inawapa mikakati mbalimbali kwaajili ya kuboresha zao hilo. 

Mkulima wa tangawizi Oscar Gabriel, amesema kutokana na zao hilo kuwa jipya mkoani humo ipo hasa kwa serikali walifanya kuwa zao la kimkakati ikiwa ni pamoja na kusaidia uwepo wa masoko ya uhakika. 

"Kama serikali italifanya zao hilo kuwa la kimkakati kwa kuhakikisha soko la uhakikika linapatikana itasaidia wakulima wengi kulilima zao hilo kwa wingi katika mkoa wetu hali itakayosaidia kujikwamua kiuchumi," amesema Gabriel. 

Mkulima kutoka wilaya ya Kasulu Magreth Siame, amesema yeye ni mara yake ya kwanza kulima zao hilo lakini ameweza kuona faida na kwamba serikali iwasaidie mikopo hata kwa riba nafuu kwa vikundi vikundi ili waweze kumudu gharama za kulima zao hilo. 

"Wakulima waligundua zao la tangawizi lina faida ninauhakika watajitokeza wengi kulima lakini kitakachowaangusha ni gharama za kulima zao hilo kuwa kubwa, kama serikali italibeba hili kwa kutupatia mikopo kwa riba nafuu hakika umaskini utabaki kuwa historia katika wilaya yetu na mkoa kwa ujumla, "amesema Siame. 

Msimamizi wa kampuni ya NOJEPACO CO LTD ya mkoani Arusha, Suzana Kavishe amesema kampuni yao ipo kwaajili ya kutoa elimu kwa wakulima wa tangawizi na kuwahudumia kuanzia mwanzo wa kilimo mpaka wanapovua mazao yao. 

Amesema anawashauri wakulima wa tangawizi kulima aina ya Zingiber ya tangawizi ambapo watakuwa na soko la uhakika kutoka kwao na kuwainulia kipato cha familia zao. 

"Wao kama kampuni kazi yao ni kununua zao la tangawizi linalolimwa na wakulima hao pamoja na kuwapimia sampuli ya udogo kwa wakulima hao kwa gharama nafuu,"amesema Kavishe

Afisa wa Kilimo mkoani hapa Jerry Abeli, amesema serikali bado inaendelea kuhamasisha wakulima wadogo kuingia katika kilimo hicho kwani kwasasa kimekuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo mengi. 
Wakulima wa zao la tangawizi wakiwa katika semina ya jinsi ya kulima zao hilo katika wilaya ya kasulu mkoani Kigoma, iliyoandaliwa na kampuni ya NOJEPACO CO LTD ya jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...