Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Umma Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Dr. Arnold Towo akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wakati wa ziara fupi katika Shule ya Lindi Sekondari. 

Mkuu wa Kitengo cha Udahili Kurugenzi ya Shahada za Awali kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Victoria Lyimo akiwapa maelezo wanafunzi wa Lindi Sekondari wakati wa Ziara fupi iliyofanywa shuleni hapo. 


Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ziara fupi iliyofanywa na Chuo hicho Agosti 7,2019. 

************* 

Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kimetembelea na kufanya mazungumzo na Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Mkoa wa Lindi. 

Akizungumza na wanafunzi hao, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Umma Dr. Arnold Towo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwataka wawe wabunifu na wenye kujituma katika masoma yao. 

Jambo la msingi sana kwenu ni kujitambua na kuchagua masomo yale ambayo yatawasaidia katika maisha yenu ya baadae. 

“Nawaomba sana mjitume na kutumia nafasi mnazopata ikiwa ni pamoja kufanya midahalo itakayo wasaidia kuwajengea uwezo wa kujieleza, hii itawasaidia pale mtakapomaliza masomo na kujiandaa na ajira”, alisisitiza Dr. Towo. 

Aidha Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Kurugenzi ya Shahada za Awali Victoria Lyimo aliwasisitiza wanafunzi hao kuwa Wachamungu, kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii kwa kuzingatia haya hata kwenye Masomo yenu mtaweza kufanya vizuri sana. 

Shule ya Lindi Sekondari kidato cha Tano na Sita inamichepuo ya HKL, HGL, EGM, PGM na HGK katika masomo haya wanafunzi wameaswa kusoma kwa bidii ili waweze kuwa nanufaulu mkubwa utakao wasaidia pindi wanapotaka kujiunga na Chuo Kikuu. 

Hii ni sehemu mojawapo ya jukumu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitengo cha Huduma kwa Umma kurudi kwa jamii kuzungumza na kutoa hamasa kwa wanafunzi mbalimbali nchini katika Masuala ya Elimu,Tafiti na Ushauri. 

Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kupitia ndaki ya Sayansi ya Kilimo na Ufugaji wa Samaki wa Kisasa kimeshiriki katika Maonesho ya Wakulima Nane Nane yenye kauli mbiu isemayo “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi” kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2019 katika Viwanjanvya Ngongo Kanda ya Kusini Mkoani Lindi ambapo kilele cha maonesho hayo ni kesho Tarehe 8 Agosti, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...