Na Karama Kenyunko-Michuzi TV

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kupigia kura vivutio vya utalii ikiwemo kuuchagua mlima Kilimanjaro na Tanzania ili kuweza kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za taasisi ya kimataifa ya world Travels Awards ya nchini Uingereza na hatimae kushinda.

Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi ametoa rai hiyo leo Septemba 23,2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya tuzo hizo ambazo sherehe zake kwa washindi zitafanyika Novemba 28, mwaka huu Muscat Oman.

Amesema, katika kinyang'anyiro hicho Tanzania kama kituo cha utalii kinachoongoza kwa safari za kitalii duniani, 2019 inashindanishwa na nchi nyingine 17 za bara la Afrika ambazo in Kenya, Botswana, Namibia, Afrika Kusini,Uganga ambia na Zimbabwe.

"Lakini kuingia tu kwenye kinyang'anyiro hicho haitoshi, jambo la maana zaidi ni kupiga kura, jambo linalotakiwa ni kushinda ili mlima wetu wa Kilimanjaro na Tanzania kama kituo cha Utalii viweze kushinda. Amesema Mdachi.

Amesema Mlima Kilimanjaro uko katika kundi la kivutio cha Utalii kinachoongoza 2019 ukiwa unashindanishwa na vituo vingine 13. 

" Mbali na mlima Kilimanjaro, Kisiwa cha Zanzibar kinashindanishwa na visiwa 18 katika kundi la Kisiwa ambacho ni Kituo cha Utalii kinachoongoza duniani pamoja na Hoteli ya Diamonds la Gemma dell'Est ya Zanzibar ambayo imeingia kugombea tuzo ya duniani katika kundi la Hotel za ufukweni zinazoongoza duniani kwa mwaka huu ikishindanishwa na hotel zingine 17," amesema.

Vituo vingine ni Thanda Island, Essaque Zalu ya Zanzibar, Beyond Mnemba Island Lodge, Chumbe Island Coral Park, Greystoke Mahale na Singita Sasakwa Lodge.

Aidha ameeleza jinsi ya kupiga kura tembelea tovuti ya taaaisi ya World Travel Awards ambayo ni www.world travelawards.com kisha unaingia katika eneo la kupiga kura kisha unajisajili, baada ya hapo utafuata maelekezo mpaka kufikia kupiga kura ambapo amewataka wananchi kuhakikisha wanaupigia kura Mlima Kilimanjaro katika kundi la vivutio vya utalii vinavyoongoza duniani. 
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Utalii (TTB),  Devota Mdachi akizungumza na waaandishi wa habari juu ya kuwepo Kinyang'anyiro cha 
 Kuwania tuzo za World Travel Awards zinazotarajiwa kutolewa Novemba 28, mwaka huu huko Muscat Oman. 
 Mwandishi wa Habari, Kibwana Datchi akielekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi namna ya kipiga kura katika kinyang'anyiro hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Utalii (TTB),  Devota Mdachi akiwaonyesha  waaandishi wa Habari namna ya kupigia kura vivutio vya Utalii vya Tanzania ukiwemo Mlima Kilimanjaro ili uweze kupenya katika Kinyang'anyiro cha Kiwania tuzo za World Travel Awards zinazotarajiwa kutolewa Novemba 28, mwaka huu huko Muscat Oman.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...