Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

SERIKALI ya Tanzania imesema imesitisha safari zake za ndege kwenda nchini Afrika kusini kutokana na machafuko yanayoendelea 
 nchini humo hadi pale watakapopata taarifa juu ya  usalama wa abiria. 

"Tutasitisha safari zote za ndege kwenda Afrika Kusini hadi pale tutakapojua kuwa serikali yetu imefanya mawasiliano na Serikali ya Afrika Kusini ili kuhakikisha kwamba usalama wa abiria watakaobebwa na usalama wa ndege tukapewa uhakika (Guarantee) ya kimaandishi kwamba abiria watalindwa na ndege italindwa ndipo tutaanza tendela na safari.

Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema hayo leo Septemba 5,2019 wakati wa uzinduzi rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) ubungo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, hawawezi kuwapeleka abiria sehemu ambayo wanajua wananchi wako hatari.

"Kwa mujibu wa ratiba, ndege hiyo ilikuwa inapaswa kesho kuruka kurudi Afrika Kusini lakini nyie wenyewe ni mashahidi kwamba nchi ile sasa hivi kuna fujo kubwa inaendelea ya vijana ambao wameamua kuchukua mamlaka mikononi, hivyo tumeona kwamba hatuwezi kuwapeleka abiria kwenye eneo ambalo maisha yao yako hatarini, tunaomba muendelee kuvuta subira", Amesema Kamwelwe.

Ameongeza kuwa pamoja na hayo, biashara itaendelea na wanafanya utaratibu kuhakikisha kwamba abiria wanaotoka Afrika Kusini na kwenda huko wataendela kupelekwa na shirika la ATCL kupitia ndege zingine kwa sababu ruti hiyo imeishasainiwa.


Amesema, ndege hiyo iliyokuwa inashikiliwa tangu Septemba 23,2019 sasa hivi iko huru na asubuhi imefanyiwa ukakuguzi sababu imekaa Afrika Kusini kama siku nane na haina madhara yotote kwa sababu imeruka vizuri na imefika usalama hivyo inatarajiwa leo majira ya saa tisa itaingia kwenye ruti za kawaida na kuanza kuruka.


Aidha amesema pamoja na ndege hiyo kuachiwa pia kuna gharama ambazo aliyekuwa ameishtaki ndege hiyo atausika nazo hivyo wanasheria wa kutoka Tanzania kwa kushirikiana na wanasheria kutoka Afrika Kusini wanafuatilia hukumu hiyo na taratibu hizo watazufanyia kazi na taarifa itatolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...