KIKAO Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar leo Septemba 20, mwaka 2019 kimepitisha jina la Ndugu Cassian Galos Nyimbo kuwa Katibu wa Idara ya Organazesheni Zanzibar.

Nafasi hiyo ilikuwa wazi baada ya kufariki hivi karibuni aliyekuwa Katibu wa Idara hiyo Marehemu Bakari Hamad Khamis.

Kikao kilikuwa cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 (2).

Uteuzi huo umefanyika chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyeongoza Kikao hicho.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 9:00 Mchana.

Pamoja na mambo mengine Kikao kimepokea na kujadili Taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM.

Imetolewa na:-

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,

Idara ya Itikadi na Uenezi CCM-Zanzibar.

Bi.Catherine Peter Nao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...