Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akiwa na viongozi wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo sambamba na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Charles James, Michuzi TV
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi amemshukuru Rais Dk John
Magufuli kwa namna alivyotekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya
kipindi kifupi.
DC Katambi amesema Rais Magufuli amefanya mambo
makubwa kwenye afya, elimu, miundombinu na miraidi ya maendeleo na
kuwataka Watanzania kuzidi kumuombea.
Amesema zawadi pekee ambayo
imekua Watanzania wanaweza kumpatia Rais Magufuli kutokana na utendaji
kazi wake basi ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa wazalendo na kuweka
maslahi ya Taifa mbele.
" Hakuna Taifa lolote duniani ambalo
limefanikiwa bila kufanya kazi siri yao kubwa kuwa na umoja wa kitaifa,
mshikamano na upendo hivyo ni vema Watanzania tukawa na upendo na
Serikali yetu hii ambayo inafanya kazi usiku na mchana kutuletea
maendeleo.
" Lakini jambo lingine na kubwa la kumpatia Rais
Magufuli ni kumwaga kura nyingi sana mwakani kwenye uchaguzi Mkuu kwa
sababu kwa haya mambo makubwa anayofanya Reli ya Kisasa, Bwawa ka Umeme,
Ndege, Ubanaji wa matumizi na kuzuia ufisadi vyote hivyo vinatosha
kumfanya asiangaike kuomba kura," Amesema DC Katambi.
Akizungumza
mbele ya kamati ya siasa ya Wilaya hiyo, DC Katambi amewaahidi
kuendelea kusimamia kwa upana maslahi ya umma na mtumishi yeyote
atakwenda kinyume na maagizo na kasi ya Rais Magufuli hatosita
kumchukulia hatua.
Amesema kwenye maeneo ya kuchukua hatua ataendelea kuchukua hatua bila kumuonea mtu.
"
Lazima tugombane tunavyoona mtu hafati misingi ya utumishi ya umma na
niwaambie watendaji na watumishi wote waliopo ndani ya Wilaya hii
sitomchekea mtu hakuna udugu wala urafiki kwenye mali za umma. Kwa
viongozi wenye kasoro mimi sina unafiki. Kabla sijatumbuliwa mimi
mwingine atakua amesagwa kabisa," Amesema DC Katambi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...