Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akizungumza na wadau wa kongamano la Kimataifa la kujadili masuala ya kijiografia(GAT)
Mtoa mada kutoka nchini Afrika Kusini akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya tabianchi na namna ya jamii unavyoweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Dk.Leonard Akwilapo akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila.
KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amefungua Kongamano la kimataifa la kijiografia, linalojulikana kama (GAT) ambao linalenga kujadili mabadiliko ya tabia nchi na namna jamii inavyoweza kukabiliana na changamoto hizo.
Akifungua mkutano huo unaofanyijka katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) jijini Dar es Salaam, Dkt. Akwilapo amesema jiografia ndiyo maisha kwa kuwa inaangalia, Kilimo, Afya, Ajira, na maisha ya kila siku.
“Elimu ndiyo mkombozi wa maisha, jiografia ni afya, Kilimo na maisha ya kila siku hivyo Jamii inavyopambana na mazingira ndivyo inavyochangia katika Kukuza uchumi wa nchi husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila ameeleza kuwa pamoja na majukumu mengine ya Chuo, Chuo pia kinawajibika kufanya tafiti hivyo kupitia Kongamano la GAT wadau wanapata fursa ya pamoja ya kujadili, kuoneshana namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitikeza katika Jamii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Mabadiliko ya tabia nchi ni changamoto ktk sekta zote, hivyo hili ni eneo ambalo wataalamu wanatoa ushauri wanamna ya kukabiliana nalo kupitia mkutano wa namna hii wa GAT” alisema Prof. Mwakalila.
Naye mmoja wa washiriki wa mkutano huo ambaye ni Mhadhiri MwandamiZi wa Chuo Kikuu Nkwawa Dkt. Evaristoo Haule amesema GAT imejikita kufanya kazi na watafiti, na wanataaluma katika masuala ya Jiografia ikiwemo watunzaji wa wanyama, utunzaji wa Maliasili, uchumi wa viwanda na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Kongamano hilo la siku tatu ambalo limeanza leo linashirikisha wadau kutoka nchi zaidi ya tano ikiwemo Afrika Kusini, Ethiopia, Nigeria, Zambia na wenyeji Tanzania.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Habari na Mawasiliano,
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...