Na Ripoti Wetu, Michuzi TV

KATIKA kutambua umuhimu wa biashara na uwekezaji nchini, viongozi wa ngazi mbalimbali wamezungumza hatua zinazochukuliwa na Serikali kuboresha huduma kwa wawekezaji na umuhimu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika kufanikishwa uwekezaji wa wawekezaji watarajiwa nchini

Viongozi hao wamezungumza hayo hivi karibuni waliposhiriki mkutano wa kusikiliza changamoto za wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa wa Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki amesema kwa sasa wanafanya maboresho katika sera na sheria ya uwekezaji ili kuwa na mazingira mazuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Ameongeza kuwa mabadiliko ya sheria ya uwekezaji yanalenga kuvutia uwekezaji zaidi na itasaidia kupunguza kiwango kinachotakiwa ili kujisajili na TIC.Pia itasaidia au kuwezesha wawekezaji wa kada ya chini na kati pia kusajiliwa na TIC.

" Usajili utawasaidia kunufaika na faida zinazotokana na kujisajili ikiwamo vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi,"amesema Waziri Kairuki na kuongeza wanategemea mapendekezo hayo yawasilishwe Bungeni Novemba, mwaka 2019.

Aidha Kairuki ameshukuru juu ya matamko mabaya ya viongozi na vitisho kwa wawekezaji na wafanyabiashara kwamba kwa sasa yamepungua na wanaomba viongozi wenye tabia hiyo waache mara moja. Pia amesema Serikali ipo kwa ajili ya kuhudumia na kufanikisha malengo ya wafanyabiashara na wawekezaji maana ndio wanatoa fedha ya maendeleo ya nchi.

"Niwapongeze Mkoa wa Ruvuma, sijawahi kusikia wala sijapokea taarifa yakuwepo kwa matamko wala vitisho dhidi ya wawekezaji bali mmekuwa wakaribishaji na wasaidizi wa wawekezaji,"amesema Waziri Kairuki.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabulla amesema wawekezaji wote wanaohitaji ardhi lazima wapite TIC hasa wawekezaji wa kigeni.

Amesema lengo ni kutengenezewa hati pacha ya umiliki yaani 'Deriverrive Right' itakayompa uwezo wa kuimiliki. Ametoa mwito kwa kwa halmashauri zote kuhimiza wawekezaji wote hasa wa kigeni wanaohitaji ardhi ya uwekezaji kupitia TIC.

"Mnapopata ardhi kwa ajili ya uwekezaji msimpe mwekezaji moja kwa moja bali fuateni taratibu na sheria za kupitia TIC ili kujiepusha na migogoro inayoweza kujitokeza pasipo na sababu.Hili lizingatiwe,"amesema.

Hata hivyo amesema Novemba 19 mwaka huu Wizara itafungua ofisi kila mkoa ili kurahisisha upatiknaji wa ardhi ikiwamo ya uwekezaji, upimaji na upatikanaji wa hati ngazi ya kila mkoa. Amesema hiyo itapunguza usumbufu kwa wawekezaji na wafanyabiashara kufuatilia hati mikoa jirani (Kanda) au Dar es Salaam.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Fedha Dk.Ashatu Kijaji amesema hakuna nchi inayoendelea bila wafanyabiashara na wawekezaji. Na ili nchi iendelee tunahitaji kodi kwa maendeleo na kodi inatokana na wafanyabiashara na wawekezaji hivyo tushirikiane nao vizuri.

"Katika kuboresha na kuweka mazingira mazuri mwa wafanyabiashara na mwekezaji inashauriwa wapewe miezi sita(6) kabla ya kuanza kulipa kodi pale wanapoanza utekelezaji wa miradi yao,"amesema.

Ameongeza kuwa hiyo itawapa muda wa kujifunza, kujitathmini na kujipanga kwa ajili ya kulipa kodi na kuongeza malipo yafanyike kupitia mashine za EFD zinazotolewa na TRA na sio vinginevyo.

Pia amesisitiza kodi kulipwa kwa utaratibu wa sheria husika na si vinginevyo, hivyo maofisa wazingatie hilo na wafuate sheria wanapokusanya kodi.

Kwa upande wa Wizara ya Mazingira imeeleza kuna uhusiano mkubwa kati ya uwekezaji na mazingira na kwamba uwekezaji wowote unaofanyika lazima uwe endelevu kwa maana ya uzingatie sheria za kutunza uhifadhi mazingira kwa matumizi ya leo na hata vizazi vinavyokuja.

Wizara hiyo imetoa mwito kwa wawekezaji wote kuwasiliana na NEMC ili kupata miongozo ya mazingira wanapotarajia kutekeleza miradi yao nchini. Aidha NEMC pia inafanya maboresho ili kumwezesha mwekezaji kupata kibali cha kuendelelea na mradi wake. 

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika Mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina  Mabula akifafanua jambo kuhusu uombaji wa ardhi kwa wanaohitaji ardhi kwa ajili ya uwekezaji
 Naibu Waziri wa Fedha Dk.Ashatu Kijaji akizungumza katika mkutano huo ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa kukufanya kodi kwa mujibu wa sheria
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...