NAIBU Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amewapatia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Samora Machel iliyopo mkoani Mbeya Kompyuta tano pamoja na mashine moja ya kisasa ya kuchapisha mitihani shuleni hapo.

Dk Tulia amekabidhi Kompyuta hizo shuleni hapo katika uzinduzi wa chumba cha Kompyuta kilichopewa jina la TULIA TRUST lengo likiwa kuwawezesha wanafunzi kujifunza masomo ya Kompyuta na kuendana na teknolojia iliyopo hivi sasa.

Katika uzinduzi huo Naibu Spika ameahidi pia kushirikiana na wadau wa elimu kuwajengea mabweni wanafunzi hao baada ya kugundua idadi yao kubwa wanaishi mitaani katika nyumba za kupanga.

Amesema pia atahakikisha anasaidia upatikanaji wa Kompyuta zingine ili kuweza kutosheleza mahitaji hayo kwani Shule hiyo ina wanafunzi wengi na Kompyuta zilizopo haziwezi kutosheleza mahitaji yao.

" Niwapongeze sana kwa kuweza kujenga chumba hichi na kuwa na wazo la kuwajengea wanafunzi hawa uwezo wa kutumia Kompyuta kwani kutawarahishia katika kuendana na mahitaji ya teknolojia.

" Nimeguswa na mwamko wenu na mimi pamoja na kutoa hizi tano na mashine yake ya kuchapia mitihani niahidi kuongeza zingine lakini pia kushirikiana na wadau mbalimbali kujenga mabweni hapa ili wanafunzi hawa waweze kuishi karibu na Shule," Amesema Dk Tulia.

Amesema Serikali inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora hivyo ni jukumu lao kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kutoa elimu bure.

“Nimeelezwa pia watoto wote hapa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wanakaa mitaani ambapo ni changamoto kwao, kwenye hili niseme tutatafuta wadau na ikiwezekana tuanze kujenga mabweni kwa ajili ya watoto hawa lakini napenda tuanze na mabweni ya watoto wa kike kwasababu hawa changamoto zao ni kubwa zaidi ukilinganisha na wa kiume ingawa tungetamani tujenge yote hivyo kwa kuanza tutaanzia hapo” Amesema Dk Tulia.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (katikati ) akikata utepea kuashiria uzinduzi wa chumba cha Komyuta kilichopewa jina la TULIA TRUST kilichopo katika Shule ya Sekondari Samora Machel iliyopo mkoani Mbeya, ili kuwawezesha Wanafunzi kujifunza masomo ya kompyuta kwa vitendo ili kuendana na teknolojia iliyopo sasa.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (katikati ) akiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Samora Machel iliyopo mkoani Mbeya, alipowasili kuzindua chumba cha Komyuta kilichopewa jina la TULIA TRUST 
Picha ya pamoja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...