ECOBANK Tanzania leo Septemba 20 imetangaza kufanya maboresho ya uendeshaji wa huduma kwa kimfumo wa kiteknolojia ili kuweza kukidhi mahitaji ya wateja na kutoa huduma iliyobora zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa kitengo cha biashara Ecobank Respige Kimati  amesema kuwa benki hiyo ipo kwenye mchakato wa kuboresha mfumo wake wa kibenki kutoka mfumo wa Flexcube 7 walioutumia kwa miaka saba na kwenda kwenye mfumo bora zaidi wa kiteknolojia wa Flexcube 12.

Amesema kuwa kuanzia Septemba 23 mwaka huu  akaunti namba za wateja zitabadilika kutoka tarakimu 16 hadi tarakimu 10 na wateja watakuwa huru kufanya huduma za kifedha kwa kutumia akaunti namba zao za awali.

Amesema sababu za kubadilisha mfumo huo ni kuongezeka kwa wateja na  mahitaji kutoka kwa wateja yamekuwa mengi na ili kuboresha kiwango katika mifumo hiyo wameona ni vyema wakabadilisha mfumo wa kiteknolojia ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.

Aidha amesema kuwa benki hiyo ambayo ni sehemu ya Ecobank group inayowafanya kazi katika nchi  ya zaidi ya 30 Afrika wamebadilisha mfumo huo ili kutoa huduma kieletroniki faafu zaidi bila huduma za kifedha kusumbua, na hatua hiyo isaidia katika kutoa huduma kwa teknolojia  zaidi mahali popote.

Kwa upande wake mmoja wa wateja wanaotumia kutoka benki hiyo  Violet Mfinanga amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na benki hiyo ni muhimu sana na wao kama wateja wanaamini itaenda kutatua changamoto katika mifumo ya kifedha .


Violet amezishauri taasisi nyingine kutumia mifumo hiyo kwa kuwa itaokoa muda na kiuchumi itasaidia kurahisisha kufanya miamala mingi ya kifedha kwa muda mfupi.
 Mkuu wa kitengo cha Biashara Ecobank Tanzania Respige Kimati akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliofika kwenye kikao cha kujadili maboresho ya mifumo ya Kibenki ya Ecobank yatakayoanza Septemba 23, 2019 yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Sumalu akiwakaribisha wateja waliofika kwenye kikao cha kujadili maboresho ya mifumo ya Kibenki ya benki hiyo yatakayoanza Septemba 23, 2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wateja wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kuhusu maboresho huduma za Ecobank yatakayoanza Septemba 23, 2019  yatakayofanikisha huduma kufanyika kwa haraka na kidijitari utaoanza kutumika Septemba 23, 2019.
Afisa wa Malipo ya kidigitali Ecobank Tanzania, Brown Kessy(kushoto) akijibu maswali ya wateja wa benki hiyo wakati wa kikao kilichowakutanisha wafanyakazi wa Banki hiyo na baadhi ya wateja kujadili maboresho ya mifumo ya Kibenki ya Ecobank yalichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Biashara Ecobank Tanzania Respige Kimati.
Baadhi ya wateja wa Ecobank pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakifuatilia mada

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...