Kampuni ya Engen Petroleum (T) Limited, imezidundua kituo kipya cha mafuta jijini Dodoma,ikiwa ni sehemu ya kujitanua na kuongeza wigo wa kibiashara kwa kuwafikia Wateja wake walioko katika maeneo mbalimbali nchini,

Akizungumza jana katika uzinduzi rasmi wa kituo hicho kilichopo barabara ya Meliwa (zamani Kilimo kwanza),Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Paul Muhato aliuhakikishia umma kuhusu upatikanaji wa soko la bidhaa za Kampuni hiyo,ikiwa ni sehemu ya uchangiaji wa kukuza uchumi jijini Dodoma na miji mingine nchini Tanzania ambako kampuni hiyo imekuwa ikijitanua .

Alisema Kampuni ya Engen Petroleum (T) Limited ni kampuni yenye mafanikiyo, iliyojidhatiti vilivyo na yenye ubunifu mkubwa,hasa katika utoaji wa huduma na bidhaa zake bora za mafuta,pamoja na maduka yanayorahisisha upatikanaji wa bidhaa bora za kampuni hiyo.

"ENGEN imekuwa mshirika katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 20 sasa,hivyo kama sehemu ya kuendeleza mkakati wake wa kujitanua kibiashara,nauhakikishia umma kuhusu uwepo wa soko la bidhaa za kampuni ya Engen zipo za kutosha,zilizo na kiwango cha ubora wa Kimataifa na usiotia shaka kabisa'',alisema Muhato.

Amesema upanuzi wa vituo katika maeno mbalimbali ni hatua ya asili katika mpango wa ukuaji wa kampuni kwa sasa,na pia wanaendelea kuangalia maeneo ya kimkakati nchini kote kwa ajili ya maendeleo na ununuzi wa vituo vya rejareja ili kutumikia vyema soko la Tanzania.

"Hivi sasa tuna vituo 10 vinavyopatikana katika mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tanga, Moshi, Arusha na Mwanza - lakini idadi hii itaongezeka katika kipindi cha miaka michache ijayo,

Tukiwa tunakusudia kuweka mteja kama kipaumbele cha kwanza, tunatarajia angalau vituo vinne zaidi katika maeneo ya kimkakati mwishoni mwa mwaka,huku tukisisitiza umuhimu wa kuwa na mafuta bora kwa wateja wetu poote pale'', alisema Muhato .

Amesema katika suala la utoaji huduma,Wana wahudumu Waliofundishwa vizuri kawahudimia wateja kwa saa 24 kila siku, lakini pia upatikaji wa malipo ya bidhaa zao,unaweza kutumia njia nyingi ikiwemo ya kwa njia ya kadi ya Mafuta ya Engen.

"Wateja pia watafurahia huduma zingine kadhaa kama vile maduka, migahawa ya hali ya juu, Sehemu ya matengenezo ya magari, mahali pa kuosha gari na huduma zingine, zote zikiwa chini ya paa moja. "alimaliza kusema Muhato.

Muoenekano wa Kituo kipya cha mafuta Engen kilichopo barabara ya Meliwa (zamani Kilimo kwanza)jijin Dodoma mjini
Madereva wa pikipiki wakisubiri kupata ofa ya kujaziwa mafuta kila mmoja waliohudhuria katika siku ya uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Engen jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...