Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili Mtaa wa Malindi kuhudhuria Mazishi ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Bibi Fatma Mbaraka Salum.
Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiisamu wakimsalia aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Bibi Fatma Mbaraka katika Msiki wa Malindi Mjini Zanzibar.
Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiisamu wakiishindikiza Maiti ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Bibi Fatma Mbaraka kuipeleka kwenye malazi yake ya kudumu Mwanakwerekwe.
Picha na OMPR -ZNZ.
ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Tekelezaji ya Mkoa Mjini Magharibi Mwishoni mwa Miaka ya 90 Bibi Fatma Mbaraka Salum aliyefariki Dunia Jana amezikwa leo asubuhi katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B”.
Bibi Fatma Mbaraka ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Malindi Mwaka1998 na kujiuzulu Mwaka 1999 alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya Kisukari na shindikizo la Damu.
Mamia ya Waumini wa Dini ya Kislamu, Wananchi pamoja na Wanachama wa Vyama vya Kisiasa kutoka maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Unguja wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Serikali walihudhuria Mazishi hayo yaliyofanyika Mtaani kwake Malindi Mjini Zanzibar.
Marehemu Bibi Ftma Mbaraka Salum alizaliwa Mnamo Tarehe 01 Oktoba Mwaka 1943 na baadae kupata Elimu yake ya Dini na Dunia kama ulivyo utaratibu wa Utamaduni wa Watoto wa Taifa hili.
Mnamo Mwaka 1964 Bibi Fatma alijiunga rasmi na Chama cha Afro Shirazy Party na kuteuliwa kufanya Kazi ya Katibu Muhtasi wa Aliyekuwa Meya wa Mji wa Zanzibar Makao Makuu ya ASP kuanzia Mwaka 1966.
Katika maisha yake kwenye Ulingo wa Kisiasa Marehemu Bibi Ftma Mbaraka Salum alikuwa Kamanda wa Jimbo la Malindi na baadae akiwa Mwanake pekee Zanzibar kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM Malindi kati ya Mwaka 2002 hadi 2007.
Mwaka 2007 hadi 2015 Marehemu Bibi Ftma Mbaraka alikuwa Balozi Nambari Moja Tawi la Chama cha Mapinduzi Malindi ambapo baadae alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee Tawi la Malindi.
Wana Mtaa wa Malindi wataendelea kumkumbuka Bibi Ftma Mbaraka Salum kama Mama Mlezi wa Mtaa huo kutokana na sifa ya ukarimu na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Jamii yote iliyomzunguuka hasa Vijana na Watoto.
Kila Nafsi itaonja Mauti kama alivyoagiza Mwenyezi Muungu Muumba wa Mbingu na Ardhi na hivyo ndivyo ilivyomkuta Bibi Fatma Mbaraka akirejea kwa Muumba wake akituacha sisi kwenye foleni ya kurejea wakati wowote kuanzia sasa kuipata haki hiyo isiyokimbilika.
Marehemu Bibi Fatma Mbaraka Salum aliyefariki Dunia akiwa na Umri wa Miaka 76 ameacha Mtoto Mmoja. Mwenyezi Muungu ampe hatma njema alikotambukia. Amin.Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
25/09/2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...