Hospitali binafsi, zahanati, vituo vya afya, wasambazaji huduma za matibabu kupata mikopo yenye bei nafuu.

Inatarajiwa kuboresha utoaji huduma za afya nchini

BENKI ya NMB imezindua huduma mpya kwa lengo la kutoa mikopo ya gharama nafuu kwa hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati iliopewa jina la 'NMB Afya loan'

Huduma hii mpya ni matokeo ya ushirikiano kati ya Benki ya NMB na shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF) ambapo NMB itatoa mikopo kuanzia Sh Milioni 2 hadi Bil 5 wakati MCF inatoa dhamana ya asilimia 50 katika mikopo yote.

Wafaidika wa Mkopo wa Afya ni hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati, maduka ya dawa na wasambazaji dawa ili kuwezesha, kuiinua na kuboresha biashara za huduma za afya nchini.

Aidha, Benki ya NMB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kuingia katika ushirikiano kama huo na MCF nia ikiwa kujenga uwezo Sekta ya Afya.

Kwa pamoja NMB na MCF watashirikiana kutekeleza ufadhili wa huduma ya afya, kupanua na kuimarisha ubora wa utoaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi.

Huduma hii itawawezesha watoa huduma ya afya kupata fedha pamoja na kupata utaalum wa kiufundi, ambao utasaidia kutambua wauzauji na vifaa vya matibabu bora pamoja na upatikanaji wa vifaa vya tiba kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mkuu wateja binafsi, biashara ndogo na za kati Filbert Mponzi alisema, huduma hiyo ya mikopo imefika kwa wakati mwafaka na utachangia kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za afya na kujenga mifumo endelevu kwasababu upatikanaji wa mitaji unakuwa rahisi zaidi.

"Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Benki ya NMB leo. Kuna fursa nyingi katika sekta ya afya nchini na sisi kama NMB, tumeliona hili na tumejikita kuwapa nafasi hospitali, vituo vya afya wasambazaji wa vifaa vya tiba kujiendeleza. Tunaimani huduma hii itachangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji mkubwa wa utoaji huduma za afya za bei nafuu, "alisema Mponzi.

Itakumbukwa, Benki ya NMB imepigiwa kura kuwa benki nzuri zaidi nchini kwa miaka saba mfululizo na tuzo za kifahari za kimataifa za Euromoney; vilevile ndio benki inayoongoza katika kufadhili biashara ndogo na za kati kwa sekta mbalimbali.

Mkurugenzi wa MCF Tanzania, Dk. Heri Marwa alisema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo mpya ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha watanzania wengi wapata huduma nafuu za afya na tiba.

"Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji ni changamoto kubwa katika nchi nyingi za Kiafrika na inazuia utoaji huduma nafuu za afya hususan tukiangalia mifumo endelevu ya afya.Kwa huduma hii tunafurahi kwamba hospitali nyingi binafsi, vituo vya afya vitapata na uwezo wa kuwekeza kwenye vifaa vya afya vya kisasa, na tunafurahi kushirikiana na benki bora nchini Tanzania kufanikisha upatikanaji wa mitaji ya biashara nchini,” alisema Dk. Heri Marwa.




Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akimpongeza Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati baada ya kuzindua huduma ya AFYA LOAN uliofanyika katika Hospitali ya Heamed Bunju jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wakubwa na wakati wa benki hiyo, Donatus Richard, Mkurugenzi Mkaazi wa Medical Credit Fund, Dk Heri Marwa na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Edwina Lupembe




Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika katika Hospitali ya Heamed Bunju jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizugumza wakati uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika leo katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam

Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati akizugumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika leo katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkaazi wa Medical Credit Fund, Dk Heri Marwa akizugumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika leo katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo


Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...