Timu ya madaktari kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha wamezindua huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito katika kituo cha afya Daraja Mbili kilichopo Jiji la Arusha.
Akiongoza zoezi hilo Dkt.Chacha amesema kuwa kuzinduliwa kwa huduma hiyo kutawapunguzia wananchi gharama kwa kuwa huduma hiyo ni bure katika vituo vya afya vya serikali ukilingalinganisha na vituo vingine.
Ameongeza kuwa licha ya kupunguza gharama kwa wananchi lakini pia kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kupunguza msongamano kwa mama wajawazito kujifungulia katika hospitali za mjini kama vile hospitali ya rufaa ya Mount Meru.
“Kwa sasa hivi huduma ya upasuaji kwa mama wajawazito inapatikana katika vituo vya afya vitatu vya Jiji la Arusha ambavyo ni Kaloleni, Levolosi na Daraja Mbili na kituo kinachofuata kuzinduliwa huduma hii ni Murriet” alisema Dkt. Chacha.
Timu ya madaktari wa kituo cha afya Daraja mbili wakiwa katika upasuaji wa kwanza wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha.
Timu ya madaktari wa kituo cha afya Daraja mbili katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha (wa tatu kutoka kulia) baada ya kukamilisha upasuaji wa kwanza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...