MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Tanzania Enlightenment Development Innovations(TEDI) Gloria Anderson amesema vijana wanapaswa kufanyia kazi ndoto zao kwani ndio wakati sahihi.

Pia amesema kama wanahitaji kuona malengo ya maendeleo endelevu yanafikiwa ni lazima vijana wenyewe wafanyie kazi malengo ambayo wamejiwekea.

Anderson ameyasema hayo juzi katika Maadhimisho ya Africa Evidence Week kwa mwaka 2019 ambapo shirika hilo lilipata nafasi ya kushiriki.Maadhimisho yamefanyika  Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. 

Akizungumzia zaidi katika lengo namba nne la elimu bora ikiwa ni lengo kuu la shirika hilo amesema kuna umuhimu wa elimu yetu kubadilika kutoka kwenye kusoma maandishi tu na kuwa ya vitendo tupo.

 "Tupo katika karne inayohitaji uvumbuzi wa vitu mbalimbali.Vijana wengi wanakosa ajira kwa sababu ya kukosa ujuzi unaohitajika, kusoma na kufaulu ni jambo moja lakini kuwa na ujuzi ni kitu kingine,"amesema. 
Ameongeza soko la ajira linahitaji watu wanye uwezo na wenye kufanya kazi kwa vitendo kupitia ujuzi walionao na kwamba mwaka 2017 alifanya utafiti kuangalia elimu ya vyuo vikuu inachangia kwa kiasi gani kuwasaidia vijana kupata ajira.

"Matokeo ya utafiti yalionesha kati ya vijana 100 vijana 36 tu ndio walifanikiwa kupata ajira baada ya kuhitimu masomo ya vyuo wengine 64 walishindwa kupata ajira kwasababu ya kukosa ujuzi unaohitajika kwenye usahili,"amesema. 

Pia amesema katika karne ya 21 soko la ajira linahitaji mtu anayeweza nini na sio anajua nini.Kwa upande wake mmoja wa wazungumzaji katika maadhimisho hayo Naamala Samson amesema vijana ni nguvu kazi inayoweza kuleta mabadiliko makubwa nchini.

"Asilimia 60 ya idadi ya watu ni vijana, hivyo ni muhimu kuhakikisha vijana wa Tanzania wanajitambua , wanatambua fursa zinazowazunguka na kuzitumia ipasavyo kujiajiri na kuajiriwa, ili kujiletea maendeleo yao binafsi na nchi kwa ujumla,"amesema.

Wakati huo huo Dk. Nelsen Amar elimu kwa wakulima inahitajika zaidi kama tunahitaji kuiona Tanzania yenye maendeleo ya viwanda tunayotaka. 

Naye Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Odemary Peter amesema wanafunzi wengi wanakosa elimu bora kwa sababu ya umasikini, mimba za utotoni na ndoa za utotoni pamoja na umbali wa wanafunzi kutoka nyumbani kwenda mashuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...