Mkurugenzi Mtendaji wa J FILM 4 LIFE, Jenifer Kyaka, al maarufu kama Odama akizungumza baada kuzindua siku ya kuanza kutafuta vipaji vya watoto watakao igiza filamu ya watoto. Siku ya kuanza kutafuta vipaji vya watoto Septemba mwaka huu 14 katika viwanja vya Club Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa J FILM 4 LIFE, Jenifer Kyaka, al maarufu kama Odama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
KATIKA kuendeleza tasinia ya filamu nchini kampuni ya J FILM 4 LIFE inaendeleza dhamila hiyo kwa kutafuta vipaji vya watoto wa kuanzia miaka mnne hadi miaka 14.
KATIKA kuendeleza tasinia ya filamu nchini kampuni ya J FILM 4 LIFE inaendeleza dhamila hiyo kwa kutafuta vipaji vya watoto wa kuanzia miaka mnne hadi miaka 14.
Mkurugenzi Mtendaji wa J FILM 4 LIFE, Jenifer Kyaka, alimaarufu kama Odama, amesema kuwa katika sekta ya filamu kwa mara ya kwanza wanampango wa kuvumbua na kukuza vipaji vya watoto hapa nchini.
“Sote tunafahamu kuwa tasnia ya filamu nchini kwetu imeendelea kukua na kuboreka hasa katika miaka ya hivi karibuni. Sisi wasanii wa Tanzania na ubora wa kazi zetu za sanaa umeimarikaa mara dufu kupelekea kuweza kuaminika zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu”. Amesema.
“Kundi kubwa la watoto wanatakiwa kushirikishwa katika jamii ili kusiwepo na ubaguzi wa kuwa umri gani unaweza kutoa ujembe kwenye jamii kupitia sanaa”. Amesema Jenifer.
Jenifer amesema kuwa tamthilia hiyo ambayo itakayohusu watoto italenga maudhui ya watoto pia na waigizaji ni watoto wenyewe ndio maana wameona umuhimu wa kutafuta vipaji vya watotoili maudhui yaendane na waigizaji.
Tamthilia hiyo italenga watoto na ikielezea zaidi maisha ya watoto katika mambo mbalimbali kama vile elimu, afya, migogoro ya kifamilia kwa watoto, dini, miradhi, mila na utamaduni pamoja na mila mbalimbali, unyanyasaji wa watoto ubakwaji watoto ikiwa pamoja na watoto wa mitaani itagusa maisha ya uhalisia wa maisha ya mtaani na familia nyingi hapa nchini.
Mchakato wa kupata watoto wenye vipaji wa kuigiza filamu ya watoto utafanyika katika viwanja vya clabu liders Septemba 14 kuanzia saa tatu kamili jijini Dar es Salaam.
Pia Jenifer amewaomba wazazi kuwaruhusu watoto wao kwaajili ya kuja kufanya usahili wa mchujo wa watoto watakasoigiza filamu hiyo. Hata hivyo amewaalika wadau wa masuala mbalimbali ya watoto kuja kukutana na wadau wengine kama wadau wa elimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...