Mratibu wa Kongamano la kuombea nchi amani kutoka Taasisi ya Mudir Markaz Safina, Sheikh Said Kinyogoli(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano hilo mjini hapa jana.Kulia ni Sheikh Najim Humoud na kushoto ni Imamu Sheikh Abubakar Masuala. (Picha Boniphace Jilili).



Na Boniphace Jilili, Singida 


Kongamano kubwa la kuiombea nchi amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mratibu wa Kongamano hilo Sheikh Said Kinyogoli alisema limeandaliwa na TaasAsi ya Mudir Markaz Safina chini ya baraza kuu la waislam Tanzania (Bakwata),lengo likiwa ni kuiombea nchi amani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Panapo kusekana amani hauwezi kufanya jambo lolote liwe la kijamii na la kimaendeleo kwani ukijaribu mara unasikia bomu linalipuka kwasababu hakuna amani." alisema Sheikh Kinyogoli.

Sheikh Kinyogoli alisema kongamano hilo litafanyika kwa siku saba katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi mjini hapa, kuanzia siku ya jumatano wiki hii na litashirikisha watu wote bila kujali itikadi za kidini, ambapo watakuwepo masheikh, Hilary Kipozeo, Hashim Mbonde na Mzee Yusuph wote kutoka Dar es salaam. 

Wengine ni Sheikh Jafari Abdulahaman kutoka Morogoro, Sheikh Mohamed Makarani-Mwanza pamoja na Sheikh Ibrahim Mlumbango kutoka Kigoma. 
Alisema sanjari na kuiombea nchi amani pia watakuwa wanaadhimisha mwaka mpya wa kiislam ambapo watatoa nasaha za kidini ili watu wawe na hofu ya Mungu.

Sheikh Juma aliongeza kuwa katika kongamano hilo yatatolewa mafunzo ya ujasiriamali kwa ajili ya watu kujifunza mbinu za kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kujiinua kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...