Posted: 14 Sep 2019 11:18 AM PDT


Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mara yanayondelea mjini Mugumu, Wilayani Serengeti. Kongamano hili linalojumuisha wadau kutoka Tanzania na Kenya, linalenga kujadili mustakabali wa bonde la Mto Mara na nafasi yake katika shughuli za uhifadhi.

Akizungumza katika kongamano hilo Balozi Mwinyi amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Kenya katika shughuli zote zinazolenga kujenga ustawi wa uchumi na jamii, na kuendeleza uhusiano imara uliopo baina ya nchi hizi mbili bila kusahau suala la uhifadhi wa mazingira ya bonde la Mto Mara.

Aidha amewataka wadau kuwa huru kutoa mawazo yao yanaoyelenga kutatua changamoto za uhifadhi zinazolikabiri bonde hilo sambamba na kuboresha jitihada na mikakati inayotumika sasa.

Kongamano hili linatarajiwa kutoa maazimio ambayo yatatoa uelekeo mpya na kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli na jitihada za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara.

Tarehe 15 Septemba, 2019 inatarajiwa kuwa siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mara yanayoendelea kufanyika mjini Mugumu wilayani Serengeti.
Meza kuu ikifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kongomano la Siku ya Mara lililofanyika katika ukumbi wa Kisarare mjini Mugumu, Serengeti


Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,akifuatilia jambo wakati kongamano likiendelea

Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, ambaye pia alikuwa mgeni wa heshima katika kongamano hilo akizungumza na hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kujadili changamoto za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akifuatilia majadiliano katika Kongamano la ‘Siku ya Mto Mara’ linaloendelea Mugumu – Sengereti Mkoani Mara. Kongamano hilo linaongozwa na kauli mbiu isemayo Nitunze Nikutunze. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima.

*****************************

Na Ibrahim Mdee, Mara.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Simamwishoni mwa wiki ameshiriki katika kongamano la mto Mara linalofanyika Mugumu Wilaya ya Serengeti.

Katika kongamano hilo Naibu Waziri Sima amekuwa Mwenyekiti katika mjadala uliohusu Utunzaji wa Mazingira na uhifadhi wa Ikolojia ya Mto Mara.Naibu Waziri Sima amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mto Mara ni jitihada zaviongozi wakuu wa nchi zetu mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya kwa upande mwingine. “Ushirikiano wao ndio unaendeleza jitihada hizi za kuutunza mto huu muhimu” Sima alisisitiza.

Akizungumzia Malengo ya Siku ya Mto Mara Sima ameainisha kuwa ni kukutanishajamii za pande zote mbili za nchi, kuona na kutambua faida za uhifadhi wa mto Mara kwa kuzingatia wajibu wa kila mmoja, kwa kuwa imebainika Bonde hilo linakabiliwa na Changamoto kubwa za uharibifu wa mazingira zitokanazo na shughuli zisizoendelevu za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na uvuvi.

“Hivyo kwa kutambua Changamoto hizi ni lazima wananchi wapewe taarifa sahihi za uharibifu na wajibu wao katika uhifadhi wa mto mara, Uharibifu ukiendelea kuna hatari ya Kupoteza ikolojia nzima ya mto Mara, hivyo mto utakauka na kusababisha atharikubwa kwa jamii na wanyama katika hifadhi yetu ya Serengeti na Maasai Mara huko Kenya” Sima alifafanua.

Imebanika kwamba takribani watu milioni 1.3 wanategemea uwepo wa bonde la Mto Mara katika shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji. Hata hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu ambalo halina uwiano na matumizi ya bonde la mto Mara, hivyo kuongezeka kwa idadi ya watu kumeongeza uharibifu wa uoto wa asili.

Aidha, imeelezwa kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na gugu vamiziambalo linaathiri mimea ya asili hasa majani ambayo yanasaidia kuhifadhi uoto wa asili ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanachangia katika uharibifu wa Mazingira katika bonde la mto Mara.

Katika majadiliano hayo imedhihirika kuwa uharibifu mkubwa Uko uwanda wa juu(upstream) maeneo ya Kenya na uwanda wa chini (downstream) na Ili kukabiliana na hali hiyo imependekezwa kuanzishwa kwa chanzo cha kudumu cha Fedha kwa ajili ya kushughulikia uhifadhi wa bonde la Mara.

Pia, watafiti wa mazingira ikiwemo taasisi za elimu kuendelea kufanya tafiti zinazoweza kuibua njia sahihi za uhifadhi wa bonde la mara ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa jamii inayoishi kandokando ya mto Mara.

Kongamano hilo limeenda sambamba na uwasilishaji wa mada zinazotilia mkazoumuhimu wa uhifadhi wa bonde la Mto Mara, na kuongozwa na kauli mbiu isemayo “Nitunze Nikutunze”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...