Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watendaji wa Manispaa zote za Jiji Dar es Salaam wakiongozwa na wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wakandarasi jijini Dar es Salaam leo.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na watendaji wa Manispaa zote za Jiji hilo wakiongozwa na wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wakandarasi wanaosimamia miradi mbalimbali ambapo amesikiliza ripoti za utekelezaji wa miradi katika halmashauri zote.

Baada ya kusikiliza miradi inayotekelezwa katika kila Wilaya na changamoto zake Makonda amesema kuwa lazima watendaji wajenge timu ya matokeo chanya na washirikiane katika kutatua changamoto.

Akizungumza leo Septemba 25,2019 jijini Dar es Salaam Makonda amesema kuwa.

"Isifike hatua hadi kiongozi mkubwa anakuja na kukuta mapungufu wakati kuna viongozi wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo, aliyekuwa ananielewa ni Hapi aliyekuwa Dc wa Kinondoni wengine wanaambiwa hivi wanafanya vile, nawahakikishia kuna watu watatokea Central kwenda kwenye kazi zao na kuna watu watahama nyumbani kwao hadi miradi ikamilike nitaongozana na RAS na kamanda Mambosasa muda wowote kuanzia leo kukagua miradi."

Aidha Makonda amewataka watendaji wa manispaa zote kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia gharama za miradi pamoja na kutumia vya ndani katika kutumia malighafi zinazozalishwa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...