Mbunge wa Singida Magharibi, Mhe Elibariki Kingu ameupokea msafara wa kundi la waandishi wa habari wanaoenda nchini Burundi kuiunga mkono Timu ya Taifa 'Taifa Stars' katika mchezo wake wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Mhe Kingu pamoja na kuupokea msafara huo wenye watu 35 pia ameuandaliwa kifungua kinywa pamoja na kuchangia kiasi cha Shilingi Laki Mbili kama sehemu ya kuunga mkono kampeni hiyo ya kuhamasisha Timu ya Taifa.

" Niwashukuru Sana ndugu zangu wanahabari kwa kuamua kujitolea kuunga mkono Timu yetu ya Taifa. Historia lazima iwakumbuke mmefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa hapo awali. Nyinyi ni mashujaaa wa Taifa hili.

" Niwahikikishie Mimi ni sehemu ya kampeni yenu, nitashirikiana nanyi kwa kila Jambo, lengo likiwa kumuunga mkono Rais wetu Dk John Magufuli kupitia Michezo na haswa Timu yetu ya Taifa. Twendeni pamoja.," Amesema Mhe Kingu.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na wandishi wa habari za michezo na ilianza katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, dhidi ya Kenya ambapo Taifa Stars ilifuzu kwenda hatua inayofuata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...