Na Daniel Mwambene Ileje
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini  vigogo wanne wa vyama vya siasa vya upinzani wilayani Ileje vimepoteza majembe yake baada ya kuhamia CCM ili kuijenga Tanzania mpya kama walivyosema.
Waliokabibdhi kadi zao za vyama vya awali kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe na kupewa kadi mpya za kijani ni pamoja na Ndg.Pitirosi Mshani aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Itumba ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Ileje.
Wngine ni Ndg.Francis Mbembela aliyegombea udiwani kata ya Isongole 2015 kupitia ACT Wazalendo akitokea CHADEMA ambako aliwahi kuwa kiongozi pia,Eliamu Kibona pia (CHADEMA) alikuwa ni mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Itumba pamoja na mama Dale Kaonga aliyekuwa tishio upande wa wanawake kisiasa akitokea CHADEMA.
Wakizungumza mara baada ya kupokelewa na Katibu wa Mkoa wageni hao waliahidi kukitumikia chamaa hiki na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu.
“Kazi zinazofanywa na Awamu hii haziwezi kupingwa kwa lolote kwani zinalenga kuwakomboa watanzania,yeyote anayepinga matokeo ya kazi hizi atakuwa anapingana na Mungu”Alisema Ndg.Eliamu Kibona.
Akizungumza na wajumbe wa kikao kwenye Ukumbi wa CCM wilayani humo(maarufu kama Kimwaga) Bi.Mecy Moleri aliwataka wanachama wa CCM kuungana na wanachama hao wapya katika kazi mbalimbali za chama ikiwemo mipango ya ushindi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Naye,Diwani wa Kata ya Itumba Mhe.Mohamed Mwala alifurahia kupokea wageni hao akisema hakika chama kimepata majembe ya kazi.
 Makatibu wa matawi  CCM Wilaya ya Ileje wakifurahia baada ya kuwapokea wageni toka upinzani.
 Wajumbe wa Kikao (makatibu wa matawi) wakisikiliza maneno toka kwa Pitirosi Mshani (hayupo pichani) mara baada ya kupewa nafasi ya kujieleza ambpo alisema amerudi nyumbani baada ya kuwa upinzani tangu 1993.

 Ndugu Francis Mbemebela (kushoto) akisalimiana  na Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe Bi.Mecy Morell mara baada ya kupokelewa akitokea ACT wazalendo

Vigogo wa upinzani Ileje walihamia CCM wa kuoka kulia ni Pitirosi Mshani (CHADEMA), Francis Mbembela ACT Wazalendo(aliyevaa tai),Eliamu Kibona(CHADEMA)Na Bi.Dela Kaonga (CHADEMA). Vigogo hao waliohamia CCM hapa wakipokea nasaha toka kwa Mwenyekiti wa  CCM Wilaya Ileje Ndg.Hebron Kibona(hayupo pichani). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...