Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA zimepita siku nne tangu mapacha Merryness na Anosia kurejea nchini kutoka nchini Saudi Arabia walikofanyiwa upasuaji mmoja wa pacha hao amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa huduma za upasuaji wa hospitali hiyo Dkt.Suphian Baruan amesema kuwa Anisia amesema kuwa pacha huyo amefariki dunia wakati wakimpatia matibabu.

Amesema kuwa tangu walivyorejea nchini Anisia alionekana kuwa na tatizo na wakaanza kumfanyia uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumpatia matibabu.

Daktari wa upasuaji wa watoto Petronilla Ngilino amesema kuwa wakati wakiendelea kumfanyia uchunguzi Anasia alianza kutapika hali iliyowashtua na mama wa mtoto huyo aliwaeleza hali hiyo ilianza tangu walivyokuwa kwenye ndege na alikuwa akiishiwa nguvu.

"Tulifanya uchunguzi pamoja na kumwekea maji kwa kuwa yalikuwa yanapungua, pia tulizuia matapishi yasiingie kwenye mfumo wa hewa lakini baada ya uchunguzi tukabaini ana tatizo kwenye tumbo utumbo ulijikunja" ameeleza Dkt. Ngilino.

Mapacha hao walizaliwa Januari 29, 2018 katika Zahanati ya mtakatifu. Thereza Omukajungutu Wilayani Misenyi na kusafirishwa Mkoani Bukoba kabla ya kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili wakiwa wameungana kuanzia kifuani hadi miguuni ambapo mfalme Salman wa Saudi Arabia alidhamini upasuaji kupitia Serikali.

Mwili wa marehemu Anisia unategemewa kusafirishwa hadi Mkoani Bukoba kwa mazishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...