Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amezitaka Wizara zinazoshughulika na masuala ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanaangaza katika matukio ya kikatili yaliyowalenga wageni nchini humo ikiwa ni pamoja na kukomesha kabisa matukio hayo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ramaphosa ameandika kuwa hakutakuwa na uhalali kwa raia wa Afrika kusini kuwadhuru watu kutoka nchi nyingine za Afrika na kueleza kuwa watu nchini humo wanatakiwa kuishi kwa amani hata kama kuna shida yoyote inatakiwa kumalizwa kwa kufuata misingi ya Kidemokrasia.

Kwa upande wa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Richard Lupembe
amesema kuwa hadi leo mchana hakuna tukio lolote la raia wa Tanzania
kudhurika kwa namna yoyote katika vurugu hizo zilizowalenga wageni.
Chombo
cha habari Cha Aljazeera kimeripoti kuwa katika mitaa ya Alexandra
polisi walionekana wakidhibiti kikosi cha watu 50 waliokuwa wanarusha
mawe.
Vurugu hizo ziliibuka jumatatu wakati vikosi vya uokoaji vikizima
moto katika jengo la Jeppestown ambapo iliripotiwa kuwa watu kadhaa
walipoteza maisha na majeruhi walipatikana, watu katika vikundi
mbalimbali waliendeleza kuvamia sehemu za biashara na kuchoma moto na
kupora huku ikielezwa kuwa waliathirika zaidi ni raia kutoka nchi za
Nigeria, Somalia na Ethiopia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...