NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ametoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, na walimu ambao shule zao zilifanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya elimu ya msingi na sekondari mwaka 2018 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2019.

Sambamba na zawadi hizo, Mhe. Makonda pia ameahidi kutoa ofa kwa walimu 30 wa jiji la Dar es Salaam wakiwa na wenza wao kwenda kwenye mbuga ya wanyama ikiwa ni furaha yake baada ya shule za jiji la Dar es Salaam kufanya vizuri kwenye mitihani hiyo lakini pia kwenye michezo ya Umiseta.

Kandoni na hafla hiyo, Maafisa wa Mwalimu Bank, benki ambayo ilikuwa miongoni mwa wadau wakubwa wa walimu kusapoti shughuli hiyo, walikabidhi kadi za ATM kwa walimu ambao ni wateja wa benki hiyo sambamba na kuandikisha wateja wapya ambao walijitokeza kufungua akaunti.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mhe. Makonda pamoja na mambo mengine aliipongeza Benki ya Mwalimu na wadau wengine kwa kuunga mkono elimu na walimu.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Bank, Bw. Richard Makungwa alisema asilimia kubwa ya wanahisa wa benki hiyo ni walimu na kuwahimiza walimu kutumia huduma za benki hiyo ili kufikia lengo la kuanzishwa kwake la kuwainua walimu kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia), akimkabidhi tuzo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa kutokana na benki hiyo kuwa miongoni mwa taasisi zilizofanikisha hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa wanafunzi na walimu wa mkoa wa Dar es Salaam waliofanya vizuri kwenye mitihani ya taifa ya elimu ya Msingi na Sekondari mwaka 2018. Hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Karume ulio katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam leo Septemba 21, 2019. Benki ya Mwalimu inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na walimu kote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa cheti kwa mmoja wa walimu wa shule ya sekondari iliyofanya vizuri kwenye mitihani hiyo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa hotuba yake.
Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa, akitoa hotuba yake.
Afisa Uhusiano wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Michael Kachala, (kulia), akimuelimisha Mwalimu huyu ambaye ni mteja wa Mwalimu Commercial Bank, namna ya kutumia ATM card. Benki ya Mwalimu iko katika mtandao wa ATM za Umoja Switch kote nchini.
Walimu wakijaza fomu za kufungulia akaunti, kandoni mwa hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao shule zao zilifanya vizurio kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ya eli mu ya Msingi na Sekondari mwaka 2018. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Septemba 21, 2019.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mwalimu Commercial Bank, Bw.Selemani Kijori (mwenye miwani), akizungumza na mmoja wa walimu ambaye alifika kwenye meza ya benki hiyo kuhudumiwa.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mwalimu Commercial Bank, (MCB)Bw.Selemani Kijori (mwenye miwani) pamoja na timu yake Afisa wa Huduma kwa wateja wa MCB, Bi.Martha Gambosi(wapili kulia) na Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw.Bw. Michael Kachala, wakichambua ATM cards za wateja wa benki hiyo tayari kuwakabidhi.
Afisa mahusiano wa tawi la Mlimani Mwalimu Commercial Bank, Barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam wa Benki ya Mwalimu Bw. Abdulhakim Salimu (kushoto), akimwelekeza mteja namna ya kujaza fomu ya kufungulia akaunti.
Elimu ya ATM card ikiendelea kutoklewa hapa ni Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw.Michael Kachala (kulia), akifafanua jambo kwa mteja
Afisa wa Huduma kwa wateja wa Malimu Commercial Bank (MCB), Bi.Martha Gambosi (kulia) akimweleza jambo Mwalimu huyu (aliyeipa mgongo camera) kuhusu huduma zitolewazo na benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...