Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na watendaji wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo wanafanya miradi ya jijini lake lisiendelee na kusababisha kukwama kwa miradi ya kimaendeleo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akiteta jambo na kipongozi mwenzie.

Baadhi ya watu waliohudhulia mkutano wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza.

Na Leandra Gabriel, MICHUZI TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewajia juu viongozi wanaofanya kazi bila kufuata mifumo ya kiutawala katika ngazi ya Mkoa na kusababisha kukwama kwa miradi ya kimaendeleo.

Akizungumza katika kikao maalumu kilichowakutanisha, wakuu wa Wilaya, wakuu wa idara, wakurugenzi, wakandarasi, washauri wa miradi na viongozi wa sekta mbalimbali Makonda amewataka viongozi hao kutoa taarifa katika ofisi husika kuhusiana na changamoto za utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Aidha Makonda ameishangaa  wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kurudisha nyuma kasi ya ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 1.5  hadi kufikia shilingi milioni 700.

"TARURA mnakusanya mapato hadi kwenye maegesho ya kwenye nyumba za watu kweli? Na bado kasi ya ukusanyaji imeshuka kutoka bilioni 1.5 hadi kufika milioni 700," ameeleza Makonda.

Makonda amesema kuwa jana Katibu mkuu TAMISEMI  na Katibu tawala wa Mkoa walikutana na baadhi ya watendaji ambapo alishiriki sehemu ya kikao hicho na walikubaliana kuwachukulia hatua watendaji ambao hawatendei kazi majukumu yao.

Kuhusiana na ujenzi unaosuasua wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti na ujenzi katika fukwe za Coco Beach Makonda amesema kuwa alikutana na viongozi wa Wilaya hizo na walipewa muda wa kukamilisha miradi hiyo.

"Tarehe 22 mwezi wa tatu nilikutana na viongozi wa  Kinondoni na niliwapa siku 3 kuanza ujenzi Coco cha kushangaza mkataba umesainiwa Julai au Agosti, hata Ilala nao nilikutana nao tarehe hiyo lakini mkataba ulisainiwa Septemba baada ya kauli ya pili au ya tatu ya Rais" ameeleza Makonda.

Katika kikao hicho Makonda amewakataa watendaji wawili na kushauri wahamishwe vituo vya kazi baada ya kusuasua katika utendaji kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...