Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe. Paul Makonda ameitisha kikao baina yake na watendaji wa Mkoa huo wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Mamea, Wakurugenzi wa Manispaa, Makatibu tawala na wakuu wa Idara ili wamueleze ni kitu gani kinachowafanya miradi ya kimkakati ikiwemo Machinjio ya Vingunguti na Ufukwe wa Coco imechelewa kutekelezwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa fedha za miradi hiyo lakini fedha hizo zimeishia kukaa kwenye Akaunti pasipo utekelezaji.

RC Makonda amesema katika mkutano huo utakaofanyika Jumatano ya September 25 Ukumbi wa Karimjee mtendaji atakaebainika kusababisha uzembe huo atawajibisha  hapohapo kwa mujibu wa sheria na wengine watazuiwa mishahara yao.

Aidha RC Makonda ametoa wito kwa Wizara ya Utumishi na TAMISEMI kutafuta njia bora ya kuwapata wakuu wa Idara wenye uwezo wa kuleta matokeo Chanya tofauti na sasa ambapo wengi wao wamepanda na kuwa wakuu wa idara kwa kigezo cha kukaa kazini Muda mrefu.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa walimu, wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika taaluma na Michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...