Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetakiwa kuzielekeza mamlaka husika kufanya maboresho katika fomu za uteuzi, upigaji kura na matokeo ya uchaguzi hususani fomu za matokeo ya uchaguzi kutaja jina la kituo cha kupiga kura.

Wito huo umetolewa na Mtandao wa Uangalizi wa Uchaguzi Tanzania (TACCEO) na Jukwa la Sera wakati wakitoa maoni yao kuhusiana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza katika mkutano na wandishi wa habari, Mwenyekiti wa TACCEO, Martina Kabisama amesema wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wanapaswa kutoa msaada na ushirikiano ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi.

Pia amemtaka Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kukasimu mamlaka ya kutoa vibali vya kuangalia uchaguzi na kuendesha elimu ya mpiga kura jwa msimamizi wa uchaguzi ngazi ya halmashauri.

" Baada ya uchaguzi, Waziri mwenye dhamana azielekeze halmashauri zote nchini kuandaa na kutoa taarifa ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa umma ikiainisha pamoja na masuala mengine ya upigaji kura, matokeo, ushiriki wa makundi maalum (vijana, walemavu na wanawake).

" Pia sanduku la kupigia kura liwekwe mahali ambapo watu wenye mahitaji maalum wanaweza kulifikia kwa urahisi," Amesema Kabisama.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Uangalizi wa Uchaguzi Tanzania, Martina Kabisama akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo wakati wakitoa tamko kuhusu kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...