Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi wa wa Kijiji cha Kalamba wilayani Kondoa, ambapo wananchi hao walimuomba awahimize Watendaji wake ili jengo la Kituo cha Afya Kalamba likamilike na kuanza kutoa huduma kwa Wanakijiji hao. 
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kalamba wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (hayupo pichani), alipokuwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent (hayupo pichani) kuhusu umaliziaji wa Kituo cha Afya cha Kalamba ambacho kitakuwa kikihudumia zaidi ya Wanakijiji 13,000 wa Kalamba na Haubi.
Dkt. Alpha Kwilasa wa Kituo cha Afya cha Busi akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji huduma zinazotolewa katika kituo hicho cha afya wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua chumba cha kuhifadhia maiti alipotembelea miradi ya Ujenzi wa Vituo cha Afya Wilayani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua chumba cha kuhifadhia maiti alipotembelea miradi ya Ujenzi wa Vituo cha Afya Wilayani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa maagizo kwa uongozi wa kijiji hukakikisha wanafuatilia kila hatua ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika vijiji vyao ili viweze kumalizika kwa wakati alipotembelea wilayani humo.



Na Josephine Majura, Kondoa


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa muda wa siku 37 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha kuwa ujenzi wa vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na Kalamba vinakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa vituo vya afya vinavyojengwa kwa fedha za Serikali katika vijiji mbalimbali Wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, ambapo alibaini kuna uzembe katika umaliziaji wa ujenzi wa baadhi ya vituo hivyo kikiwemo Kituo cha Afya Kalamba.

Alielezea kutoridhika na utendajikazi wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo katika usimamizi wa miradi hiyo muhimu kwa wananchi wakati Serikali ilikwishatoa fedha zote za kukamilisha miradi hiyo na kuagiza hadi Oktoba 30 mwaka huu miradi hiyo iwe imekamilika.

“Dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli yakuleta milioni 400 kwenye kituo hichi cha Afya ni kupata huduma lakini hatujaanza kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya mwaka sasa”, alisema Dkt. Kijaji. 

Aliiagiza Ofisi ya Mkoa na Wilaya hukakikisha wanafuatilia vizuri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inayofadhiliwa na Serikali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa sababu Serikali haianzishi mradi mpya bila kutoa fedha zote za miradi husika. 

Serikali ilitoa fedha kwa nyakati tofauti kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa vituo vya afya vitano wilayani Kondoa kati ya vituo hivyo, vituo viwili vya Mauno na Busi vimekamilika, huku vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na Kalamba havijakamilika. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent alimuahidi Dkt. Kijaji kutekeleza magizo yote aliyoyatoa hasa ya kulipwa kwa watumishi waliofanya kazi mbalimbali kwenye vituo hivyo vya afya ndani ya siku 14. 

Naye Mwanakijiji wa Mauno Bw. Haji Selemani, ameishukuru Serikali kwa juhudi mbalimbali inayofanya katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa huduma za jamii na kusifia huduma inayotolewa na Watumishi wa Kituo cha Afya Busi. 

Kwa upande wake Mwanakijiji cha Bereko Bw. Juma Saidi amempongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kwa kazi kubwa anayoifanya jimboni huko na kumuombea afya njema ili awe na nguvu yakufanya kazi na zaidi. 

Dkt. Ashatu Kijaji alikuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani Kondoa, mkoani Dodoma ambapo ametembelea mradi wa Ujenzi wa vituo vitano vya afya wilayani huyo ambavyo vinajengwa kwa fedha za Serikali na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakazi wa Wilaya ya Kondoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...