TAASISI ya kitazania ya Foundation for Civil Society imepongezwa kwa kuwa mstari wa mbelea katika kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Kitanzania.

Pongezi hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kigamboni, Nobert Kamugisha baada ya Taasisi hiyo kufadhili mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wilayani humo yanayoratibiwa na Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Tanzania Association of Women Certified Accountant(TAWCA).

Kamugisha alisema kuwa ni jambo la kujivunia kuona kuwa kumeanza kuwa na mwamko kwa watanzania kujisimamia wenyewe katika kuendesha mambo yetu badala ya kusubili kila kitu kutoka kwa wahisani.

“Hili ni jambo la kuungwa mkono kuoana kwamba kuna Taasisi ya kizalendo ambayo imeweza kuchukua hatua ya kufadhili ukabilianaji wa changamoto za watanzania baladala ya kungoja kila wakati watu kutoka nje.

“Kwani hatujui kuwa watu hao wanapokuwa wanawahoji wanajamii wetu wanakuwa na lengo gani jingine mbali na hilo, hivyo ni sisi kama serikali ya kigamboni tushirikiana na taasisi hii yenye lengo ya kuwakomboa wanawakem kifikra kupitia kampeni yake ya bado naweza,” alisema Kamugisha.

Katika hatua nyingine Kamugisha alizitaja changamoto zinazoikabili kata ya kigamboni na wilaya kwa ujumla kuwa ni uongezeko la vitendio vya ukatili, mimba za utotoni na ukosefu wa elimu ya kujisimamia kwa kina mama.

“Kupitia kampeni hii ya bado naweza inayolenga kuwainua wanawake wakiwamo wale waliopoteza matumaini tunaimani kuwa tunaweza kurejesha mwanga mwingine kwa jamii yetu,” alisema.

Upande wake, Tumaini Lawrence ambaye ni Mkurungezi Mtendaji wa TAWCA alisema wameamua kupelekea mradi huo wenye kauli mbiu ya bado naweza Wilayani humo kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa elimu kwa wanawake ambao wamekuwa wakikata tamaa ya kutimiza malengo yao kutokana na sababu mbalimbali.

“Tumeamua kuleta mradi huu Kigamboni kutokana na kubaini kuwa kuna uhitaji mkubwa wa elimu, kwani wasichana wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao baada tu ya kupata ujauzito, lakini pia akina mama wamekata tamaa baada ya kufanyiwa unyanyasaji kwani wengi wao wanesema kuwa waume zao wamekuwa wakiwageuza kuwa vitega uchumi.

“Pia tunahitaji kutoa elimu kwa wazazi ili kuwalinda watoto na ndoa za utotoni ambazo pia zimekuwa zikiongezeka wilayani humu, kwani tunaamini kuwa wazazi wakiwezeshwa kupata elimu basi itakuwa rahisi hata kwa familia kujikwamua na changamoto zinazoweza kuepukika,” alisema Tumaini.

Mradi huo unafadhiliwa na shirika la Kitanzania la Foundaton for Civil Society.
 Mkurugenzi mtendaji wa TAWCA,Tumaini Lawrence akitoa neno kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jana.

  Baadhi ya maafisa maendeleo wa Manispaa ya Kigamboni walioshiriki kwenye hafla hiyo wakifuatilia mjadala.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kigamboni, Nobert Kamugisha akifuatilia majadiliano hayo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...