Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa taarifa kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia litakalofanyika Septemba 24 -27 jijini Dar es salaam
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki Tamasha la 14 la Jinsia litakalofanyika Septemba 24 hadi 27 mwaka huu katika Viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo jijini Dar es salaam.
Tamasha hilo likaloongozwa na Mada kuu 'Mwanaharakati wa Jinsia Mbioni Kubadilisha Dunia' limeandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake na usawa wa kijinsia na wanaharakati binafsi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumapili Septemba 22,2019,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi amesema washiriki wa tamasha hilo ni pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka ndani na nje ya nchi,viongozi mbalimbali kutoka ngazi ya halmashauri na serikali kuu,wanaharakati na wananchi.
"Tamasha la Jinsia la Mwaka huu lina umuhimu wa kipekee kwani kitaifa na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpangokazi wa Beijing ambapo kilele chake ni mwaka 2020.Kwa njia moja au nyingin maandalizi ya mkutano wa Beijing yalikuwa chachu kubwa ya kuanzishwa na kuimarishwa kwa asasi nyingi zinazotetea haki za wanawake ",alisema.
"TGNP ni mojawapo ya asasi iliyoleta chachu kubwa ya kuunganisha wadau mbalimbali kutoka vikundi vya wanawake,wanazuoni na mitandao ya wanawake kupata sauti ya pamoja katika ushiriki wa mkutano wa Beijing,hivyo TGNP inaendelea kusherehekea uwepo wake kwa zaidi ya miaka 25 sambamba na maadhimisho ya mkutano wa Beijing",alieleza Liundi.
Alisema Tamasha hilo linatoa fursa kwa asasi za kiraia zilizoshiriki katika mchakato wa Beijing kutakafari na kusherehekea uwepo wa asasi hizo kwa zaidi ya miaka 25 ambapo azimio na mpango kazi Beijing ndiyo iliyoweka misingii ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kidunia.
"Kipekee Tanzania itakumbukwa katika historia ya kuweka misingi ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake kwani katika mkutano wa Beijing,Balozi Mhe. Getrude Mongella aliibuka kidedea kwa Katibu Mkuu wa mkutano huo wa kihistoria hali iliyoiinua Tanzania katika ramani ya dunia",alisema Liundi.
"Katika kuendelea kuenzi na kuthamini mchango wa Mama Getrude Mongella,TGNP na Tapo la Ukombozi,tumeamua kumchagua Balozi Mhe. Dr. Getrude Mongella aliyeongoza mchakato wa Beijing na pia mchakato wa 'Kuileta Beijing Nyumbani' kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Jinsia mwaka huu",alifafanua Liundi. Hata hivyo Liundi alisema mgeni maalum kutoka serikalini atakuwa Naibu Waziri- Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mhe. Dr Faustine Ndugulile.
Alibainisha kuwa tamasha hilo litahusisha mawasilisho,mijadala ya pamoja,maonesho na warsha,kusherekea mchango wa mashujaa wanawake katika kufikia haki na usawa wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo katika ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2019 likalofanyika Septemba 24 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia. Kushoto ni Mwanachama wa TGNP Mtandao Rehema Mwateba. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao Aseny Muro.
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia 2019. Amesema Tamasha hilo litahudhuriwa pia na wageni mbalimbali kutoka Afrika Kusini,Rwanda,Burundi,Eswatini 'Swaziland', Kenya,Uganda,Ghana na Zimbabwe.
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema Tamasha la Jinsia 2019 litaongozwa na Mada kuu ''Mwanaharakati wa Jinsia Mbioni Kubadilisha Dunia' na mada ndogondogo ambazo ni 'Miaka 25 ya kujenga vuguvugu la Kifeministi 'kukabiliana na mfumo dume na utandawazi',Uongozi wa Kifeministi 'Mikakati na kujenga Tapo ka Ukombozi wa wanawake',Utengenezaji,uzalishaji na usambazaji wa maarifa ya Kifeministi ndani na nje ya tapo la ukombozi wa wanawake kimapinduzi na kuendeleza tapo la ukombozi wa wanawake 'Ajenda yetu,mikakati yetu,mustakabali yetu'.
Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Mwenyekiti wa Bodi TGNP Mtandao Aseny Muro akifafanua kuhusu Tamasha la Jinsia na masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia.
Mwanachama wa TGNP Mtandao Agripina Mosha akielezea kuhusu masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia.
Mwanachama wa TGNP Mtandao Rehema Mwateba akielezea kuhusu masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia.Wa kwanza kushoto ni Afisa Programu - Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...