Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sarah Msafiri amewaomba viongozi wa dini wa wilaya  hiyo  kuilinda amani iliyopo nchini kwa  kuepuka kutoa matamko yanayoweza kuihatarisha.

Ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati  akizungumza katika mkutano wa hadhara katika  kata ya Kimbiji na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuilinda amani hiyo iliyodumu nchini tangu taifa lilipopata uhuru wake Mwaka 1961.

 Msafiri amewaomba  viongozi wa dini kuzidi kuwa chachu ya amani na kutumia nafasi waliyonayo katika jamii kwa kuwashawishi wananchi kudumisha amani ambayo ni tunu toka kwa mwenyezi Mungu.

Katika mkutano huo, Msafiri  amesema kuwa dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha ya kila siku ya binadamu, nakutaja kuwa hiyo ndiyo sababu ya serikali kuheshimu na kutambua mchango wa dini.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sarah Msafiri (kulia)akizungumza na wananchi wa kata ya Kimbiji kuhusu viongozi wa dini wa wilaya hiyo kuhakikisha wanailinda amani ya nchi,na kuepuka kutoa matamko ambayo hayafai, leo Jijini Dar es alaam katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kushoto) akisikiliza kero mbalimbli za wananchi katika ziara  yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...