Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akimsikiliza mmoja wa maafisa BASATA mara baada ya kutembelea banda la baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) katika Maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za Afrika Mashariki la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.
KUTUNZA utamaduni wa Taifa ni pamoja na mavazi na lugha hii ni tofauti kwa Tamasha la JAMAFEST linalounganisha nchini za Afrika Mashariki linalotangaza utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki na mwenyeji wa tamasha hilo hana vazi linalotambulisha utamaduni wa Tanzania.
Kwa upande wa Lugha Tanzania imekuwa mstari wa mbele kutangaza Lugha ya kiswahili na kuenea nchini nyingi za Afrika na hata mashariki ya mbali, hata hivyo imeonekana kwenye mitandao ya kijamii watu kutoka mabara mengine kuongea na kuimba kwa kutumia lugha ya kiswahili.
Tangu mwaka 2004 kumekuwa na harakati za Tanzania kutaka kuwa na vazi lake la taifa, lakini juhudi hizo zinaonekana kushindikana, huku sababu za msingi zikishindwa kuwekwa wazi na wahusika.
Suala la vazi la taifa ni muhimu sana kwa lengo la kujenga utaifa na kutambulika kwa haraka kwa raia wa Tanzania, hasa anapokuwa nje ya nchi na pia kutangaza utamaduni wa Mtanzania.
Mwandishi wa MICHUZI BLOG ametembelea banda la Baraza la sanaa la Tanzania (BASATA) katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutaka kujua vipi mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi kutokana na kuwa tupo kwenye tamasha la utamaduni na sanaa kwa nchi za Afrika Mashariki?
Hata hivyo Afisa Tehama wa Baraza la sanaa Tanzania, Rajau Sorro amesema kuwa mchakato wa kupatikana kwa vazi la Taifa punaendelea na ifikapo mapema mwakani (2020) mchakato huo utakuwa umeisha na tutakuwa na vazi rasmi la Taifa.
Nae Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema kuwa watanzania watumie tamasha la JAMAFEST kutangaza lugha ya Kiswahili pamoja na utamaduni wa Tanzania.
Matumaini ni kuwa Tamasha la JAMAFEST litakapofanyika kwa maranyingine hapa nchini tutakuwa na vazi rasmi la taifa bila shaka kwani mchakato wake umebakia miezi michache.
Matumaini ni kuwa Tamasha la JAMAFEST litakapofanyika kwa maranyingine hapa nchini tutakuwa na vazi rasmi la taifa bila shaka kwani mchakato wake umebakia miezi michache.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za Afika Mashariki linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akimsikiliza mfanyakazi wa TBC amaye alikuwa akielezea chaneli ya utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) iliyopewa jina la Tanzania Safari Channel mara baada ya kutembelea Maonesho ya Utamaduni na Sanaa kwa Nchi za Afrika Mashariki la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 21 hadi 28,2019.
Kikundi cha Sanaa cha Lumumba Threatre wakitumuiza katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vikundi vya sanaa vikijiandaa kutumbuiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...