Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo September 23 ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Stand mpya ya kisasa ya Mabasi ya Mikoani na Nchi za Jirani ya Mbezi Luis ambayo ujenzi wake umefikia 35% hadi sasa na Kumtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati.

RC Makonda amesema ujenzi wa Stand hiyo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 ambapo ndani yake kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Jengo la Abiria,Utawala, Maegesho ya mabasi 500, Shopping Mall, Hotel, Maegesho ya Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe,Vyoo, Kituo cha Polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.

Aidha RC Makonda amemuelekeza katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda Kamati ya kufuatilia Maslahi ya wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika miradi ya kimkakati ili kuhakikisha wanapata stahiki zao zote ikiwemo mishahara na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Pamoja na hayo RC Makonda ameendelea kuwataka wakandarasi wa miradi mbalimbali kuhakikisha wananunua vifaa kutoka kwenye Viwanda vya wazawa jambo litakalosaidia kuinua uchumi wa Viwanda na Taifa kwa ujumla.


Katika Ziara hiyo RC Makonda ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...