Ofisa wa Misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)John Selestine (katikati)akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Wakala huo lililopo katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wananchi wa Dar es Salaam waliotembelea banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Tamasha la JAMAFEST wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Misitu wa Wakala huo John Selestine.
 Baadhi ya mabango ya matangazo ya hifadhi za misitu ya asili iliyopo nchini yaliyopo katika Banda la TFS katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Ofisa Nyuki kutoka TFS Juma Mdoe(kulia) akizungumza katika tamasha la JAMAFEST ambapo amesisitiza wananchi kujikita kufuga nyuki ili kupata asali na mazao yake 
 Ofisa Nyuki kutoka TFS Juma Mdoe akisisitiza jambo wakati anazungumzia umuhimu wa wananchi kujikita katika ufugaji Nyuki nchini.
Ofisa Nyuki wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Juma Mdoe  (anayeandika) akiwa na Ofisa wa Misitu wa Wakala huo John Selestine kwenye banda lililopo katika tamasha la JAMAFEST

Na Said Mwishehe, Michuzi Blogu
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umewasisitiza Watanzani kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za mazingira ya asili yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini kwetu ambako kunavivutio vya utalii ambavyo vingine havipatikani mahali pengine kokote.

Kwa kutambua umuhimu wa kutangaza hifadhi hizo na vivutio vyake, TFS imeamua kupiga kambi katika Tamasha la Utamaduni na Sanaa za Nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki(JAMAFEST)linaloendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa wa Misitu kutoka wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania John Selestin amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza rasilimali za hifadhi za misitu ya asili nchini na kuongeza katika eneo la Urithi wa dunia wao wanajivunia uwepo wa misitu ya  hifadhi ya asili ambayo ni sehemu ya urithi.

"Katika urithi wetu tunajivunia uwepo wa misitu ya hifadhi za mazingira ambayo inapatikana katika maeneo mbalimbali nchini . Katika misitu yetu ya asili kuna mimea na viumbe ambavyo havipatikani sehemu nyingine yoyote zaidi ya kwetu Tanzania,"amesema Selestine na kuongeza kuwa uasili wa misitu hiyo unatokana na viumbe na mimea ya asili iliyomo.

Ameongeza kuwa TFS katika urithi wa dunia wapo katika tamasha hilo kwa ajili ya kuelezea na kutangaza misitu ya hifadhi ya mazingira asilia  ambayo imezaliwa kutokana na misitu ya hifadhi ambayo wanaisimamia na hiyo  misitu iliyotokana na tafiti mbalimbali kubaini kuna mimea na viumbe ambavyo havipatikani mahali kokote duniani.

"Uwepo wa viumbe na mimea ambavyo havipatikana kokote ndio imesababisha tuwe na urithi na kufanya misitu hiyo ya pekee .Tunawaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kutembelea misitu hiyo ya hifadhi ya mazingira ya asili ambayo nchini kwetu ipo 17,"amesema.

Amefafanua kuna maeneo mengi ya hifadhi ya mazingira ya asili ikiwemo, Amani, Magamba, Chome na Pugu.Ndani ya misitu hiyo kuna vivutio vya utalii kwani kuna mimea na viumbe vya asili ambavyo vipo kwenye hifadhi hizo. 

Pia kuna maporomoko ya Kalambo mkoani Rukwa pamoja na Ziwa Ngozi ambalo limetokana na kreta na ziwa hilo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika ambayo yanatokana na kreta.

"TFS ambayo ndio wasimamizi wa hifadhi za  misitu na rasilimali za misitu, ukweli misitu hiyo bado imeonekana inausili na vivutio mbalimbali ambavyo ni vya urithi.Tunatoa mwito kwa wananchi kujenge utaduni kutembelea hifadhi ya misitu ya mazingira ya asili,"amesema.

Kwa upande wake Ofisa Nyuki kutoka TFS Juma Mdoe ametumia tamasha hilo kuendelea kuhamasisha wananchi kujikita katika ufugaji nyuki na mazao yake kwani kuna faida nyingi ikiwemo ya kipato.

"Pamoja na kusimamia usimamizi na kuendeleza rasilimali za misitu bado wakala wetu  umejikita katika ufugaji wa nyuki na mazao yake ikiwa pamoja na kutoa elimu ya kuhamasisha wananchi kufuga nyuki kwani kuna faida nyingi,"amesema.

Mdoe ametumia nafasi hiyo kueleza mazao yatokanayo na ufugaji nyuki yamekuwa yakiingiza kipato kikubwa kwa wafugaji na kwa taifa kwa ujumla, hivyo ametoa rai kwa wananchi kujihusisha na ufugaji nyuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...