Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo leo Septemba 28,2019


TGNP Mtandao imetambulisha rasmi mradi wa Sauti ya Wanamke na Uongozi Tanzania 'Women's Voice and Leadership - Tanzania' utakaotelezwa kwenye mikoa 9 kwa lengo la kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania, vikundi na Taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuwezesha wanawake na wasichana na kuongeza ulinzi wa haki za wanawake na wasichana kufikia usawa wa kijinsia.

Mradi huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitano 'Aprili 2019 hadi Machi 2023' kwa ufadhili wa Global Affairs Canada (GAC) umetambulishwa rasmi leo Jumamosi Septemba 28, 2019 kwa washiriki wa mradi waliohudhuria Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika kikao cha kutathmini Tamasha la Jinsia la 14 kilichofanyika kwenye ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. 

Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Wanawake na Uongozi Tanzania, Shakila Mayumana amesema mradi huo utatekelezwa katika mikoa tisa ambayo ni Dar es salaam, Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Mara na Kigoma. "Tulichagua mikoa ambako TGNP inafanya kazi zake, lakini pia kwenye maeneo yenye vuguvugu na yale yaliyosahaulika.Na hii inatokana na masuala tunayofanyia kazi ikiwemo sekta ya maji, afya, elimu, kilimo na uziduaji 'mafuta, gesi na madini' na Ukatili wa Kijinsia", alisema Mayumana. 

Aliwataja walengwa wakuu katika mradi huo kuwa ni watu binafsi, jamii, taasisi na vikundi vya wanawake na kubainisha kuwa pia makundi ya jamii ya wafugaji, wawindaji na wanaoishi kwa kula matunda, mizizi na asali pia yameongezwa kwenye mradi huo. Mayumana alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na kuwahamasisha wanawake kudai haki zao ikiwemo kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi. Kwa upande wake, Mwanachama wa TGNP Mtandao, Rehema Mwateba alisema mbegu ya mabadiliko inaanzia kwa mtu mmoja mmoja huku akiwasisitiza wanawake kusimamia ukweli katika kudai haki kwani ukweli siku zote unashinda.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. Mradi huo utatekelezwa katika mikoa tisa nchini Tanzania. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akitambulisha mradi huo kwa washiriki wa mradi waliohudhuria Tamasha la 14 la Jinsia 2019. Wanaharakati hao wa haki za wanawake wanatoka mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Shinyanga,Dodoma,Kilimanjaro,Mtwara,Mara na Kigoma.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akielezea malengo ya mradi huo.Alisema lengo la mradi ni kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania,vikundi na Taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuwezesha wanawake na wasichana na kuongeza ulinzi wa haki za wanawake na wasichana kufikia usawa wa kijisia. 
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiandika dondoo muhimu wakati wa kutambulisha mradi wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania.
Kulia ni Mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto mkoani Mbeya Flora Mlowezi akichangia hoja wakati wa kutambulisha mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Mwanachama wa TGNP Mtandao,Rehema Mwateba akichangia hoja wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Same mkoani Kilimanjaro,Abdulrahman Mfuru akiwasisitiza wanawake kuomba mikopo inayotolewa kwenye halmashauri ili wainuke kiuchumi.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiandika dondoo muhimu wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania kutambulishwa leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania kutambulishwa leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...