Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akizungumza wakati wa kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi za wizara ya Kilimo wakifatilia hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi kilichoitishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhabdisi Mathew Mtigumwe akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Kilimo kwa ajili ya kufungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali imesema kuwa inaendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi wanaobainika endelea kubainika wakijihusisha na vitendio ovu vya rushwa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 17 Septemba 2019 wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea.

Alisema kuwa serikali inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipambanua kukabiliana na wala rushwa hivyo yeyote anayebainika hakutakuwa na huruma badala yake atapelekwa mahakamani.

“Wenyeviti na Wakurugenzi msipoisaidia serikali kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaotoa au kupokea rushwa maana yake na ninyi ni sehemu yaw ala rushwa na kama sio sehemu lazima tuchukue hatua”

“Nimeyasema haya hadharani sina lengo la kumtishia mtu yeyote katika hili badala yake nimelisema ili hatua zichukuliwe” Alisisitiza Mhe Hasunga
Ni lazima kukumbuka kuwa wajibu mkubwa wa watumishi ni kuhakikisha kuwa dira inafikiwa kwa mujibu wa mkakati uliowekwa.

Mhe Hasunga amesema kuwa wizara ya Kilimo itapimwa katika ammbo makubwa matano, ambayo ni kuongeza uzalishaji wa chakula na tija katika kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Jambo la pili ni kwa namna gani wizara imewezesha upatikanaji wa fedha za kigeni jambo huku jambo la tatu ikiwa ni kupimwa kuwa kilimo kinakuwa kwa asilimia ngapi na kinachangia kiasi gani kwenye pato la Taifa.

Jambo la nne alilolitaja Mhe Hasunga ni kuhusu upatikanaji wa malighafi sahihi kwa ajili ya viwanda nchini, huku jambo la tano ikiwa ni kipimo cha idadi ya ajira zitakazokuwa zinapatikana kwenye sekta ya kilimo, huku jambo la sita ikiwa ni namna ushirika utakavyokuwa umeimarika pamoja na usimamizi madhubuti wa ardhi kwa ajili ya kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji.

Mhe Hasunga alisema kuwa endapo maeneo hayo matano yatafanyiwa kazi ipasavyo ni wazi kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kabisa kukibadilisha kilimo kuwa cha kibiashara na sio cha kujikimu.

Alisema kuwa maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Tasnia ya Ushirika nchini itaimarika baada ya kuzinduliwa mfumo rasmi wa mauzo ya mazao ya kilimo kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

TMX ina lengo la kuongeza ufanisi katika juhudi za Serikali za kurasimisha mifumo ya masoko ambayo imekuwa na changamoto kwa muda mrefu; kwa kuwaunganisha Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa, kuleta ushindani kwenye bei, kupunguza gharama za uendeshaji biashara na kuweka uwazi.

Amesema kuwa mbali na soko la bidhaa pia kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kielektoniki wa usajili wa wakulima na mfumo wa kielekroniki wa Kusimamia Biashara (Agricultural Trade Management Information System – ATMIS) utaimarisha makusanyo ya maduhuli na tozo kwa kuhakikisha huduma zote za utoaji vibali, leseni na vyeti unafanyika kielektroniki na pia kudhibiti udanganyifu katika hati na nyaraka za huduma hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...