Na Vero Ignatus,Arusha.

Benki ya Biashara Afrika (CBA ) imeanza kutoa mikopo ya ujenzi kwa ajili ya kuwawezesha wateja wake kuweza kujenga na kumiliki nyumba kwa kupata mkopo rafiki ambao utawawezesha kujenga na kulipa kwa urahisi.

Akizungumza katika siku maalumu ya Wateja wa benki hiyo (customers day) Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko amesema kuwa wanatoa mikopo ya ujenzi kulingana na uwezo wa mteja kulipa mkopo ,pia kulingana na faida anazozipata mteja katika biashara yake ,mkopo huo umeangalia mahitaji ya wateja wao ya kumiliki nyumba za ndoto zao.

Kwa sasa pia tuna mikopo maalumu kwa Wafanyakazi walioko serikalini ili waweze kunufaika na fursa za mikopo iliyoko katika benki zetu” Anaeleza Mkurugenzi huyo.Anasema kuwa wameanzisha huduma maalumu kwa ajili ya watalii kupata huduma za kifedha kubadilisha fedha za kigeni pamoja na huduma nyingine za kifedha.

Mkuu wa Idara ya wateja binafsi ,Julius Konyani anaeleza juu ya siku ya leo ambayo wanakutana na wateja wetu tunawashukuru kwa biashara wanayotupatia na kupata mrejesho juu yale ambayo benki yao inafanya.

Julius alisema kuwa Wateja wao wanahitaji makazi ya kudumu walihitaji kuwa na viwanja na kuanza ujenzi ,tunawakopesha mkopo wa kununua viwanja na kujenga wanaulipa kwa miaka 20.
Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko akizungumza na wateja waliohudhuria katika siku hiyo maalum
Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko akifafanua jambo kwa wateja waliohudhuria kwa siku maalumu ya mteja Benk hiyo.

Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko na wafanyakazi wa Bank hiyo.



Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya CBA .
Mkutano unaendelea .
Wafanyakazi na wayeja wakifiatilia kwa makini kile kinachoendelea katika mkutabo huo.
Wateja wa CBA Bank wakifuatilia mkutano kwa makini.
Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko akimkabidhi zawadi ya Tv mmoja wa wateja wa wateja wa Bank hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...