Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Tanga

UONGOZI wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Tanga Cement mkoani Tanga kimesema kinajivunia mafanikio waliyonayo yakiwemo ya kuendelea kutengeneza saruji ya kiwango cha ubora wa kimataifa na kuwa na soko la uhakika.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, uongozi huo umesema pamoja na kuingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania(TRC), kuna changamoto ya uchache wa mabehewa kwa ajili ya kusafirisha saruji jambo ,hivyo wametoa rai ya kuongeza mabehewa japo 300.

Hayo yameelezwa wakati ziara ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambao wamepata fursa ya kutembelea kiwanda hicho kuona shughuli mbalimbali za uzalishaji, kupata taarifa za mafanikio na changamoto.

Akizungumza jana mkoani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Reinhardt Swart amewaambia waandishi wa habari kiwanda kinajivunia kuendelea kuzalisha saruji iliyo bora ukilinganisha na washindani wao kwa kuwa na viwango vya ubora wa Kimataifa na hivyo kuwa na soko la uhakika.

"Mkakati wetu siku zote ni kuendelea kuzalisha saruji inayokidhi viwango vya ubora wa kimataifa.Gharama tunazotumia ni kubwa katika uzalishaji ambazo zinatokana na umeme, mafuta na klinka ambayo inatumika wakati wa kutengeneza saruji kiwandani,"amesema Swart.

Alipoulizwa kuhusu usafiri wa kutumia reli kusafirisha saruji, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema mara nyingi wamekuwa wakipata changamoto ya kutokuwepo kwa mabehewa ya kutosha ambapo hali hiyo inasababisha kiwanda kushindwa kufikisha sokoni zaidi ya tani 10,000 - 15,000 kwa mwezi.

Amefafanua kwamba changamoto hiyo inasababisha kuongezeka kwa bei ya saruji kutokana na kukosekana kwa bidhaa sokoni.Hata hivyo amesema ni nafuu na rahisi sana kusafirisha saruji kwa kutumia reli na kuongeza kuwa inakuwa nafuu zaidi endapo unasafirisha mzigo maeneo ya mbali zaidi. 

"Ni rahisi kwa upande wa kampuni na kwa upande wa serikali pia kwani matumizi ya reli yanapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa barabara hivyo kufanya miundombinu ya umma kubaki salama. Ukweli uliopo kama kampuni tunapendelea zaidi matumizi ya reli,"amesema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa mwezi kiwanda kinahitaji zaidi ya mabehewa 455, hivyo kama watapata mabehewa 300 yatakayojikita kwao itakuwa heri zaidi na kilio cha kutokuwepo kwa mabehewa kitapungua.

"Tunaweza kupeleka mabehewa 40 kutoka Tanga mpaka Arusha ndani ya wiki moja. Kila behewa linaweza kubeba tan 40 za saruji,"amesema wakati anafafanua kwa waandishi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart akiwaeleza Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda chicho mwishoni mwa wiki,namna wanavyojivunia mafanikio waliyonayo yakiwemo ya kuendelea kutengeneza saruji ya kiwango cha ubora wa kimataifa na kuwa na soko la uhakika.Picha na Michuzi JR.

Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda cha Tanga Cement wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart alipokuwa akiwaeleza shughuli mbalimbali zifanywazo na Kiwanda hicho,mwishoni mwa wiki.


Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa wa Kiwanda cha Tanga Cement wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kikao hicho kilichowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swart ambaye alieleza mambo mbalimbali yahusuyo kiwanda hicho.


Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart wakati alipokuwa akizungumza.
Mmoja wa Wahariri akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga,Reinhardt Swart.

Baadhi ya Wakuu wa vitengo na maofisa wa Kiwanda cha Tanga Cement wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kikao hicho kilichowakutanisha Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali, Waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho,Reinhardt Swart ambaye alieleza mambo mbalimbali yahusuyo kiwanda hicho.Picha na Michuzi JR.
Meneja Rasilimali Watu wa Kiwanda cha Tanga Cement,Diana Malambugi akifafanua ni namna gani Kampuni hiyo imekuwa ikitoa ajira katika ngazi mbalimbali za Idara za Kiwanda hicho,ikiwemo na namna ya kuhakikisha mambo ya jinsia yanazingatiwa huku akibainisha kuwa Katika kiwanda hicho suala hilo limezingatiwa vilivyo.
Mhandisi Gadiel Benjamin wa Kiwanda cha Tanga Cement akionesha sampuli za udongo na madini ya aina ya Limestone yanayotumika kutengenezea Saruji. katika kiwanda hicho wakati alipotoa mada kuhusu uzalishaji wa Saruji,mbele ya Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali pamoja na waandishi waliotembelea Kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Kiwanda cha Tanga Cement ,Nuru Mtanga akifafanua jambo na kuwashukuru wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kutokana na namna wanavyotoa ushirikiano kwa kiwanda hicho.

Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Tanga Cement ,Logolieki Mollel akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari nama saruji inavyochanganywa kitaalamu na hatimae kuipata Saruji iliyo bora na yeye kiwango cha Kimataifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...