Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini Humphrey Shao akizungumza na Vijana Wakati wa maaadhimisho ya Msakuzi Kaskazini ya Kijani.

Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi wa Kata ya Magomeni ambaye ni Muwakilishi wa Iddi Azan akitoa salamu kwa vijana.

Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini,Haroun NKanjamba akisoma Lisala kwa Mgeni rasmi.

Vijana walioshiriki katika mkutano wa Msakuzi Kaskazini ya Kijani wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti.
……………….
Na Mwandishiwetu
Wito umetolewa kwa vijana kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa,ili kuwa kuwa sehemu ya kuipatia jamii maendeleo na sio kulalamika
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini Humphrey Shao alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Msakuzi Kaskazini ya Kijani uliyofanyika katika Viwanja vya CCM Makamba.
“Huu ni Wakati wetu vijana hakuna kulalamika na kuwa wabeba mabegi kwa watu ambao wameshindwa kutatua kero zetu za muda mrefu,sisi kama kundi muhimu kwenye jamii,shime vijana sasa tujitokeze tuchukue fomu na tugombee tuwaoneshe namna ya kutatua matatizo ya jamii yetu”amesema Shao.
Shao ametaja vijana wengi wamekuwa wakirudi nyuma katika nafasi mbalimbali kwa kutishwa ama kuamini kuwa uongozi ni wa Kundi la wazee jambo ambalo Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli amelipiga Vita.
“Rais Magufuli ametuamini Vijana ndio maana katika awamu hii ya tano wapo vijana wengi waliopewa dhamana na wanaendelea kufanya vizuri hivyo sasa tujitokeze tokeze kwa wingi kila mtu katika mtaa wake” Amesema Shao.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Mbezi,Marry Biita ameagiza vijana wote kuendelea kusimama imara na kuyasema yale yote yaliyofanywa na Rais wetu Dk.John Pombe Magufuli katika Kata yetu na nchi nzima kwa ujumla.
Biita ameweka wazi kuwa maboresho ya miundombinu katika Kata ya Mbezi ni zawadi tosha kwa vijana wa CCM katika kata hiyo ambao watapata fursa ya kujiongezea kipato na kujiajiri.
Ametaja mradi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani utapokea watu zaidi ya 5000 kwa siku katika kata ya Mbezi, hivyo vijana wakae tayari kuhudumia kundi hilo kubwa ili uchumi wetu uzidi kukua .
Nae Mgeni rasmi katika mkutano huo Mh Idd Azzan kupitia mwakilishi wake aliahidi aidi jezi na kiasi cha shilingi laki tatu mara baada ya kununua keki ya Harambee kwa ajili ya ujenzi na maboresho ya ofisi ya chama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...