Mmoja ya wadau wa sekta ya  nishati jadidifu akichangia jambo wakati wa kikao cha wadau wa nishati jadidifu waliokutana leo jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wadau wa sekta ya nishati jadidifu wakijadiliana wakati wa kikao cha wadau hao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam ambacho limeandaliwa na FORUMCC kwa ufadhili wa HIVOS katika kufanikisha matumizi ya nishati jadidifu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la FORUMCC Euster Kibona (katikati)akiwa katika majadiliano kuhusu nishati jadidifu wakati wa kikao cha wadau wa nishati hiyo waliokutana leo jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Munna akizungumza jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya nishati jadidifu waliokutana leo jijini Dar es Salaam
 Meneja Programu kutoka Shirika la FORUMCC Angella Damas (katikati) akichangia jambo wakati wa kikao cha wadau waliokutana kujadiliana kuhusu nishati jadidifu
 Mkurugenzi wa FORUMCC Rebecca Munna (wa kwanza kushoto)akishiriki kwenye kikao cha wadau mbalimbali kujadili nishati jadidifu
Jophilline Bejumula kutoka asasi ya Climate Action Network Tanzania ( wa pili kushoto) akichangia mada wakati wa kikao cha majadiliano kilichowakutanisha wadau waliokutana kuweka mikakati kuendeleza nishati jadidifu nchini Tanzania kama sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.



 Na Said Mwisehe,Michuzi TV

WADAU zaidi ya 30 kutoka katika asasi za kiraia na taasisi za Serikali ambazo zinafanya kazi moja kwa moja katika nishati jadidifu nchini Tanzania wamekutana kwa ajili ya kuchambua upitiaji wa tafiti mbalimbali ambazo zimechanganua changamoto zinayoikumbuka sekta ya nishati jadidifu.

Pamoja  na mambo mengine  wadau hao wametumia nafasi hiyo kujadiliana mambo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha nishati jadidifu inapewa kipaumbele ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza kuhusu kukutana kwa wadau hao Meneja Programu kutoka Shirika la FORUMCC ambao ndio waaandaji wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es Salaam Angella Damas amesema kuwa wamekutana ili kuchambua na kupitia tafiti ambazo zimechanganua changamoto zinazozikumba sekta ya nishati jadidifu Tanzania.

Alipoulizwa kwanini nishati jadidifu, Angella amesema kuwa mbali na uwezekano wa kuisha kwa nishati kama mafuta, mabadiliko ya tabia nchi yanapelekea dunia kulazimika kutafuta nishati kupitia njia ambazo ni endelevu (sustainable). 

"Nishati jadidifu inatoa fursa ya kupunguza kuchafua dunia, na pia inazi-address changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi- kwa mfano, umeme wa grid kama ule unaotumia maji unaweza kukabiliwa na mapungufu kukitokea ukame, ila nishati jadidifu zina njia nyingi za kupatikana kama umeme wa jua, upepo na geothermal hivyo zinatoa fursa mbadala.

Ameongeza kwa kutambua umuhimu huo wa nishati jadidifu, ndio maana FORUMCC imeamua kuwakutanisha wadau hao na kisha kubadilishana uzoefu, kupeana mawazo na kubwa zaidi kujadiliana kwa pamoja na hatimaye kutoka na sauti ya pamoja ambayo italeta mabadiliko chanya katika nchi yetu hasa kwa kuzingatia nishati jadidifu ina faida kubwa sana na umefika wakati wa kupewa kipaumbele.

Pamoja na mambo mengine wadau hao wamejadili namna ambavyo masuala ya jinsi wanavyoweza kuingizwa katika eneo hilo la  nishati jadidifu huku wengine wakitoa rai kuwa ni vema kuaangaliwa upya kwa sera ya nishati na hasa ambayo itajikita katika nishati jadidifu ambayo itawasaida watoa maamuzi na viongozi wa kisiasa kushiriki kikamilifu kuendeleza nishati hiyo nchini ikiwa ni sehemu ya chachu ya maendeleo.

Hata hivyo kwa mujibu wa FORUMCC ni kwamba moja  wa mradi ambao wanausimamia unahusu nishati jadidifu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo katika hilo ni kuhakikisha nishati safi iwe inamhusu kila mtu na kwamba nishati ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo katika nchi na mkutano huo umewakutanisha wadau hao kupitia Shirika la HIVOS ambao ndio wafadhili wa nishati jadidifu.

Awali wakati akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa   Bodi ya FORUMCC Euster Kibona amesema maoni na mawazo ya  wadau ni muhimu katika kuhakikisha nishati jadidifu inapewa nafasi na hiyo ni pamoja na kuibua  mijadala itakayokuwa na tija kwa jamii kuhusu matumizi ya nishati jadidifu.

"Suala la nishati ni muhimu katika maendeleo na hivyo bila majadiliano hatutafika katika mahali.ambapo tunatamani, tumeamua majadiliano kuhusu nishati jadidifu yawe huru na tuna kila sababu ya kushirikiana kwa pamoja na lengo ni kuwa na mpango wa pamoja kuhusu nishati jadidifu."amesema Kibona.

Wakati huo huo wadau mbalimbali wametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa kuhakikisha changamoto zilizopo katika eneo la sekta ya nishati jadidifu zisiwe sababu ya kukwamisha mipango na mikakati yao katika kuendeleza matumizi ya nishati hiyo.


Pia wamesema wakati wanatamani  kuhusu nishati jadidifu wameshauri kuwepo kwa haja ya kuweka mikakati ya kuhakikisha elimu kuhusu matumizi ya nishati jadidifu inapaswa kipaumbele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...