Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said akiwasilisha maada kuhusu Matumizi ya Teknolojia katika kuendeleza demokrasia mbele ya Wanachama wa Jumuiya hiyo katika hoteli Madinat Al Bahr Business and Spa Visiwani Zanzibar.
Makamu wa Rais wa kwanza Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Tawi la Zambia, Mhe. Dkt. Evans Chibanda akizungumza wanachama wa jumuiya hiyo wakati wa semina ya Matumizi ya Teknolojia katika kuendeleza demokrasia katika hoteli Madinat Al Bahr Business and Spa Mjini Zanzibar. Kulia ni Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Rebecca Kadaga na Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said
Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Rebecca Kadaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Tawi la Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said (kulia) na Makamu wa Rais wa kwanza Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Tawi la Zambia, Mhe. Dkt. Evans Chibanda baada ya semina kuhusu Matumizi ya Teknolojia katika kuendeleza demokrasia iliyofanyika leo katika hoteli Madinat Al Bahr Business and Spa Mjini Zanzibar.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE ZANZIBAR).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...