Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akizungumza na wananchi katika uwanja wa Azimio
Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akiwa na viongozi wengine wakipasha misuli kabla ya mbio kuanza.
Mshindi namba moja wa mbio kilometa 20 Fillingson Singyi akiwa amekamilisha mbio hizo.


Na Ripota wetu, Katavi 

Wakazi wa mkoa wa Katavi kwa mara ya kwanza wamejitokeza kushiriki mchezo wa mbio za riadha za kilometa 20, kilometa 10, 5, 3 na 1 zinazojulikana kwa jina la Homera Marathon kwa lengo la kuchangia fedha za ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi inayokabiliwa na uchakavu mkubwa

Mbio hizo zimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ambaye amewataka wakazi wa mkoa huo kuchangia hospitali hiyo“Tuna namba za simu na akaunti za benki ambazo kila mwananchi anaruhusiwa kuchangia” alisema Homera

Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wameeleza dhana nzima ya mbio hizo kuwa ni pamoja na kuimarisha afya pia itaboresha miundombinu ya hospitali hiyo

Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo sasa inatumika kama Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ilijengwa tangu mwaka 1952 inakabiliwa na uchakavu mkubwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...