Na, Editha Edward-Tabora 

Zaidi ya walimu mia moja kutoka shule za sekondari kumi na tisa nchini wameanza kupewa mafunzo ya Lugha ya Alama Ikiwa ni moja ya Mpango wa Serikali na wadau wa elimu nchini kufanya maboresho katika Sekta ya elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususani viziwi

Akizungumza katika mafunzo hayo maalumu ya kujadili Changamoto mbalimbali zinazowakabili Watu wenye mahitaji maalumu yaliyofanyika katika chuo kikuu cha AMUCTA, naibu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia dkt. Avemaria Semakafu amesema wanafunzi wenye mahitaji maalumu wamekuwa hawafanyi vizuri katika Masomo yao ya darasani na kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa kutokana na walimu wanaotoa elimu kwa wanafunzi hao kutokuwa na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wanafunzi hao wenyeahitaji maalumu

"Tunatakiwa suala hili tulichukulie kiuhalisia na Tunatakiwa tuwawekee hawa wanafunzi wenye mahitaji maalumu mazingira wezeshi ili waweze kufanya vizuri katika Masomo yao na waendelee mbele ili waweze Kushiriki katika kujenga Taifa hasa viziwi pindi wanapokuwa darasani sisi kama wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia na wadau wa elimu ambao tumepewa jukumu la kusimamia suala la sera na mustakabali Mzima wa elimu bado tunasema uziwi bado ni Tatizo"Amesema Semakafu

Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa wa Tabora Suzan Nusu amesema mafunzo hayo ya Lugha ya Alama yamekuja wakati muafaka kwani yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi hao wenye uhitaji maalumu hapa nchini

"Kupitia mafunzo haya watoto hawa sasa watapata maarifa ya kutosha na tutaepukana na ile adha na aibu ambayo ilikuwa inatunzunguka mara kwa mara kwamba watoto wenye wetu walikuwa hawafanyi vizuri hasa kwa hawa ambao wana matatizo ya kutosikia nina amini kabisa tukiyatumia ipasavyo mafunzo haya hii tabia tuliyokuwa tunaiona kama Siyo kuimaliza kabisa basi tutakuwa tumeipunguza kwa asilimia kubwa"Amesema Suzan

Hata hivyo mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku kumi na nne hapa mjini Tabora Ikiwa bado Lugha ya Alama ni changamoto kubwa katika Sekta ya elimu hapa nchini na, wadau wa elimu na jamii wanapaswa kuona umuhimu wa kuwasaidia Watu wenye uhitaji maalumu hasa walio na uziwi.
 Pichani ni naibu katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu Akizungumza na walimu Wanaofundisha Lugha ya Alama nchini( Pichani hawapo).
Pichani ni walimu Wanaofundisha lugha ya Alama kutoka shule za sekondari kumi na tisa nchini walioudhuria mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...