Na Said Mwishehe,Michuzi TV
RAIS Dk.John Magufuli anatarajiwa kutunukiwa tuzo maalum kutoka kwa wananchi wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutambua kazi zake anazofanya nchini za kusimamia vema rasilimali za nchi.
Pia anatarajiwa kukabidhi Kitabu ambacho kitakuwa na maneno bilioni moja ambacho kitabeba maudhui aina mbili ikiwemo maneno ya kumshukuru Rais Magufuli kutokana na uhodari wake wa kuwa ujasiri,uzalendo uthubutu na uadilifu kwa taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Wananchi kwa Rais,John Magufuli, Nazzar Nicholas ,amewaambia wandishi wa habari leo Septemba 4,2019 jijini Dar es Salaam kuwa lengo la kutoa tuzo hiyo maalum ni kutambua mchango wake kwa wananchi katika kusimamia rasiliamari za taifa kwa ujasiri mkubwa.
Amefafanua kuwa katika mchakato wa shughuli kadhaa zitatekelezwa na wananchi kuelekea siku maalum ya tuzo hizo ambapo inatarajiwa kutolewa Septemba Mwakani.
"Mchakato huu hadi kuja kutolewa kwa Tuzo hiyo utachukua muda miezi 12 kufikia kilele ambayo siku hiyo ndio tutamkabidhi Rais Magufuli Tuzo hiyo ambayo itaendana na shughuli mbalimbali za wananchi katika kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili,"amesema Nicholas
Ameongeza kwamba miongoni mwa shughuli ambazo zitatekelezwa kipindi hicho ni pamoja na shindano maalum la kutatua kero ya wananchi ambapo wananchi watakaa na kutafuta kero inayowasumbua na kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka.
"Kutakuwa na Shughuli za uandishi wa kitabu cha Tuzo ya Wananchi kwa Rais.Magufuli,kutokuwa na Shindano la kuchora picha ya Rais,Shindano la Insha ya Wanafunzi juu ya Uzalendo kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari,Tamasha la vijana kumwombea Rais na kuwepo kwa Rais Magufuli Uzalendo Cup,"amesema
Wakati huo huo Mjumbe wa Kamati ya Tuzo hizo,Mohamed Ngoma ameomgeza hiyo ni tuzo ya kwanza kutolewa kwa Rais Magufuli kutokana na usimamizi wa rasilimali za nchi.
"Tutapita mikoa mbalimbali nchini kuangalia ni maeneo yapi ambayo Wananchi watakuwa wametatua kero zao wenyewe bila kusubiri serikali na maoni yao tutahakikisha tunaingiza katika kitabu hicho tutakachomkabidhi Rais Magufuli siku tunayompa Tuzo,"amesisitiza Ngoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...