Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

SERIKALI ya Mkoa wa Arusha imekemea tabia ya baadhi ya watu wanaofanya vitendo vya ngono na wanafunzi kwani tabia hiyo imekuwa ikisababisha mimba za utotoni na hatimaye kukwamisha ndoto za wanafunzi hao katika maisha.

Akizumgumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amesema wenye tabia hiyo ya kujihusisha na vitendo vya ngono na wanafunzi waache tabia hiyo mara moja.

Mwaisumbe aliyekuwa katika mahafali ya 10 katika Shule ya Msingi Arusha Alliance iliyopo jijini hapa amesisitiza Serikali haitavumilia kuona vitendo hivyo vinaendelea na itawachukulia hatua kaliza kisheria wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu dhidi ya wanafunzi.

"Waacheni wanafunzi wasome kwa manufaa yao ya baadaye.Kwanini wawafuate watoto wadogowakati wako watu wazima ambao wako na
uhitaji wa kuolewa na mnaishi nao huko mitaani,"amesema Mwaisumbe.

Pia amewasihi wanafunzi kuzingatia maadili mema waliyofundishwa shuleni hapo na kuacha kujihusisha na makundi maovu mitaani ikiwemo vitendo vya ngono na utumiaji wa madawa ya kulevya.

"Jitahidi sana kwenye masomo na kujiendeleza kielimu kwani elimu mliyoipata hapa ni mwanzo tu wa safari ya kimasomo ambayo iko mbele
yenu kwani mtatakiwa msome hadi vyuo vya elimu ya juu na kutimiza ndoto mlizojiwekea katika maisha,"amesema.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ArushaAlliance Silas Msuya amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 18 na sasa imefikisha wanafunzi 800.

Amesema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 133 wamehitimu na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wakawe mabalozi pindi watakapokuwa majumbani kwao wakisubiri matokeo ya mtihani.
Mkuu wa Wilaya yaLongido,Frank Mwaisumbe alipokuwa akizungumza  kwa niaba ya mkuu wa mkoa katika mahafali ya kumi ya shule ya msingi ya Arusha Alliance iliyopo jijini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...