Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizindua  Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo, Wanaoshuhudia ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Mwenyekiti wa Bodi ya UTT Amis Bw. Casmir Kyuki , Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)Bw. Nicodemus Mkama wakizindua Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)Bw. Nicodemus Mkama mara baada ya uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam, wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala na Mwenyekiti wa Bodi ya UTT Amis Bw. Casmir Kyuki. 
 KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akisoma hotuba fupi mbele ya Wageni waalikwa na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis,uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama akizungumza mbele ya Wageni waalikwa na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis,uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waageni waalikwa mbalimali wakifuatilia tukio hilo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo
..........................................................

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amezindua mfuko mpya wa uwekezaji wa pamoja ujulikanao kama Mfuko wa Hatifungani (Bond Fund) unaomilikiwa na Kampuni ya UTT-AMIS, wenye lengo la kuwawezesha wawekezaji wadogo na wakubwa kutoka ndani na nje ya nchi kuweka akiba, kukuza mitaji na kipato chao.

Akizindua Mfuko huo Jijini Dar es Salaam, Bw. James ameiagiza Kampuni ya UTT-AMIS kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili wananchi wengi zaidi wanufaike na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki uchumi wa chi yao.

Alisema kuwa UTT-AMIS inamiliki mifuko mitano yenye thamani ya sh. bilioni 300 ikiwa na wawekezaji 145,000 pekee ikilinganishwa na idadi kubwa ya watanzania.

“Namba hii ni ndogo na jitihada kubwa inahitajika ili kuwafikia watu wengi zaidi, hivyo nawaelekeza muendelee kutoa elimu kwa wananchi na wadau wengine wote ili mifuko hii iwe chachu ya maendeleo nchini” alisema Bw. James

Alitoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kuchangamkia fursa za kuwekeza katika Mfuko huo mpya wa Hatifungani kwa kuwa ni salama na una faida kubwa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala, alisema kuwa mwekezaji anaweza kuwekeza kwenye Mfuko huo mpya kuanzia sh. 50,000.

“Mwekezaji atakaye wekeza sh. 10,000,000 atapata gawio kila mwezi, atakaye wekeza sh. 5,000,000 atapata gawio la mara moja kila baada ya miezi sita wakati watakaowekeza sh. 50,000 na zaidi watapata fursa ya kukuza mitaji yao” alisisitiza Bw. Migangala

Alifafanua kuwa Bond Fund ni uwekezaji wa pamoja uliowazi ambao utawekeza kwenye hatifungani za Serikali, hatifungani za mashirika na uwekezaji katika masoko ya fedha lengo kuu likiwa ni kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika soko la mitaji

UTT-AMIS inasimamia na kuendesha mifuko mingine mitano ikiwemo Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi.

Nae Afisa Mtendaji  Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),Bw.Nicodemus Mkama amesema kuwa hafla hiyo inaweka historia kubwa katika maendeleo ya Masoko ya mitaji hapa nchini,kwani uzinduzi wa mfuko huo utatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza kwenye dhaman mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatifungani za Serikali Kuu na hatifungani za kampuni binafsi.

''Hivyo basi napenda kutumia fursa hii kuipongeza bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa UTT AMIS pamoja na Taasisi na Wadau wote waliohusika katika kufanikisha hatua hii Muhimu",alisema .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...